Home LOCAL SERIKALI KUBORESHA MAENEO YA MAKUMBUSHO YA WAPIGANIA UHURU NCHINI

SERIKALI KUBORESHA MAENEO YA MAKUMBUSHO YA WAPIGANIA UHURU NCHINI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Serikali itaendelea kuyalinda, kuyasimamia, kuyatangaza na kuyaboresha maeneo ya Makumbusho ya Wapigania Uhuru ili kuyafanya yawe vivutio vya utalii.

Ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu maswali kuhusu namna ya kukarabati miundombinu na kuboresha makumbusho ya wapigania uhuru.

Amesema kupitia fedha za UVIKO-19 kiasi cha shilingi bilioni 2.45 Serikali itakarabati miundombinu ya barabara na kuboresha maeneo ya Makumbusho na Malikale ili kuvutia Watalii.

Akifafanua kuhusu ujenzi wa barabara ya kwenda Kituo cha Makumbusho ya Mkwawa amesema Wizara ya Maliasili na Utalii itashirikiana na wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) wa Mkoa wa Iringa kuifanyia ukarabati barabara hiyo.

Aidha, kuhusu ukarabati wa Jengo la Chifu Adam Sap Mkwawa amesema Wizara inaendelea kufanya mazungumzo na familia husika ili litumike kwa ajili ya kuhamasisha Utalii.

Previous articleWAJIMAMA WAANZA NA MAMA NA MTOTO KIZIMKAZI
Next articleTAMWA-ZNZ YATANGAZA AWAMU YA PILI TUZO ZA WANAHABARI ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here