Home LOCAL OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA MAFUNZO YA UJUZI TEPE (SOFT SKILLS) KWA...

OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA MAFUNZO YA UJUZI TEPE (SOFT SKILLS) KWA MAKUNDI MAALUM YA VIJANA MANISPAA YA SHINYANGA

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe akizungumza jambo wakati wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022.

 

Sehemu ya Vijana Waliohudhuria Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, Waviu na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa lengo la kuwajengea uelewa kwenye masuala hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022.

  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana Godfrey Massawe akitoa Elimu kwa Vijana wakati wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, Waviu na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022.

Kaimu Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto kutoa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Pudentiana Rwebangira akitoa mada inayohusu Afya ya Uzazi kwa Vijana wakati wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, Waviu na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022.
 
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana Atupokile Elia akitoa Elimu kwa Vijana wakati wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, Waviu na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022.

Afisa Uendelezaji Biashara Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoani Shinyanga Joseph Taban akitoa mada inayohusu Ujasiriamali na Masoko wakati wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, Waviu na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU,

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) imetoa mafunzo ya ujuzi tepe ‘Soft Skills’ kwa makundi maalum ya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yenye lengo la kujitambua na kujithmini.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika kuanzia leo Jumanne Juni 28,2022 hadi Juni 30,2022 katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe amezitaja miongoni mwa mada zitakazofundishwa ni pamoja na kujitambua kama wajasiriamali, ujasiriamali na masoko.

Mada zingine ni urasimishaji wa biashara na usimamizi wa fedha, afya ya uzazi na ujinsia,afua zilizopo kwa ajili ya vijana wenye ulemavu na mama wadogo,afua zilizopo kwa ajili ya vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

“Vijana hawa pia watapewa mafunzo kuhusu fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi ngazi ya taifa na mkoa, fursa za mitaji na huduma kwa wajasiriamali zinazotolewa Wataalamu kutoka taasisi mbalimbali, stadi za uongozi, taratibu za uundwaji wa vikundi,uundwaji wa vikundi vya uzalishajimali vya vijana, kubainisha mahitaji ya vikundi na uandaaji wa andiko mradi”,ameongeza Tweneshe.

MWISHO

  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here