Home LOCAL KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WHO KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA

KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WHO KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA

 

Na:Catherine Sungura,WAF-Dodoma

Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Dkt. Ted Chaiban anatarajia kuja nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Julai 2022

Akizungumza na Waziri wa Afya Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania   Dkt.Zabulon Yoti amesema  kuwa Kiongozi huyo anatarajia kuwasili nchini kwa ziara ya siku nne kuanzia  tarehe 4 hadi 7 mwezi ujao ambapo atapata nafasi ya kutembekea Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Dodoma

Amesema lengo la ziara hiyo hapa nchini ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na masuala mengine ya Afya.

Wizara ya Afya hivi karibuni ilizindua kampeni ya Global Vax Initiatives yenye lengo  la kuhamasisha jamii kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na kufuatilia wale ambao hawakukamilisha chanjo zenye dozi mbili.

Previous articleAFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA TEMBO AKITOKA SHAMBANI
Next articleOFISI YA WAZIRI MKUU YATOA MAFUNZO YA UJUZI TEPE (SOFT SKILLS) KWA MAKUNDI MAALUM YA VIJANA MANISPAA YA SHINYANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here