Home ENTERTAINMENTS NIKALEX YAPATA BARAKA KUANDAA MISS DODOMA 2023

NIKALEX YAPATA BARAKA KUANDAA MISS DODOMA 2023

NA: MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Nikalex chini ya mkurugenzi wake Alexanda Nikitas, imepata heshima ya kuandaa shindano la Miss Dodoma mwaka 2023.

Huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa kampuni hii kuandaa shindano hilo tokea mchuano huu uwe chini ya The Look Campan Limited.

Akizungumza na ukurasa huu mkurugenzi wa kampuni hiyo Alexandar Nikitas, amesema mwaka huu amepanga kufanya mabadiliko makubwa hivyo anaomba wadau wajitokeze kudhamini.

“Shindano hili ni moja ya tasnia inayo kuza na kuibua vipaji vya wasichana ndiyo sababu kila mwaka najitokeza kuchukua uwakala naomba wadau, makampuni na tasisi za serekali wajitokeze kutupatia udhamini ili kufanikisha ndoto za mabinti,” anasema Alexanda Nikitas.

Aliongeza kuwa Dodomo ni moja ya mikoa ambayo imekua ikitoa warembo wazuri ambao wana iwakilisha vizuri katika jukwaa la Miss Tanzania na kuwa mabalozi na kuanzisha kampeni mbalimbli ikiwemo ya utuzaji wa mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here