Home LOCAL MTOTO AUWAWA GEITA MWILIWAKE WAKUTWA UMETUPWA PEMBENI YA MTO.

MTOTO AUWAWA GEITA MWILIWAKE WAKUTWA UMETUPWA PEMBENI YA MTO.


Na: Costantine James, Geita.

Jeshi la polisi Mkoa wa Geita linachunguza mauaji ya Mtoto wa miaka 14 Johnson Thomas mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Buhalala wilayani Geita  aliyekutwa ameuwawa na Mwili wake kutupwa pembeni ya mto.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amedhibitisha kutokea kwa mauaji hayo asema jeshi hilo linafanya uchunguzi  ili kubaini chanzo cha  mauaji.

Mwaibambe amesema baada ya uchunguzi mwili wa mtoto huyo ulikutwa umetupwa pembeni ya mto ukiwa na majeraha kwenye mguu wa kushoto huku ukiwa umepondwa na kitu kizito ambacho mpaka sasa hakijafahamika.

Amesema mpaka sasa uchunguzi unaendelea juu ya tukio hilo na hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa na jeshi  la polisi juu ya mauaji ya mtoto huyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa famila ya mtoto huyo Theophil Mkwata amesema mtoto huyo alipotea majira ya jioni tarehe 12.6.2022 aliondoka nyumbani kwenda kuandaa nguo za shule kwa fundi tangu hapo hakurudi tena nyumbani.

Amesema wao kama familia wameliachia jeshi la polisi mmoani Geita kwa lengo la kufanya uchunguzi utakao saidia kubaini chanzo na sababu za mauaji ya mtoto huyo.

Naye Padiri Salvatory Magangila paroko msaidizi parokia ya bikira maria jimbo kuu katoliki  la Geita amesema sababu ya mauaji ya mtoto kunasababishwa na  imani kushuka kwa wananchi hali inayopelekea kutenda vitendo hivyo amewataka wananchi kumcha mungu na kuachana na vitendo hivyo.

Kwa upande wa wakazi wa Buhalahala wilayani Geita wamesikitishwa na mauaji ya mtoto huyo wamelitaka jeshi la polisi mkoa wa Geita kufanya uchunguzi juu ya mauaji hayo ili waliohusika wafikiswe katika mikono ya sheria kwa lengo la kutokomeza mauaji kama hayo ndani ya mkoa wa Geita.

Previous articleSIMBA WAMTEMA WAWA
Next articleFEDHA ZA CSR ZA BARRICK BULYANHULU ZAFANIKISHA MIRADI MIKUBWA YA SEKTA YA ELIMU NA AFYA NYANG’HWALE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here