Home LOCAL MFANYABIASHARA SINGIDA ADAIWA KUMTEKA MFANYAKAZI WAKE KWA MIAKA 10 NA KUPORA...

MFANYABIASHARA SINGIDA ADAIWA KUMTEKA MFANYAKAZI WAKE KWA MIAKA 10 NA KUPORA NYUMBA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, akizungumza na Wananchi wa Manispaa ya Singida kwenye mkutano wa kusikiliza kero zao uliofanyika juzi katika Viwanja vya  Stendi ya Zamani
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi, Paskas Mulagiri akizungumza kwenye mkutano huo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida, Onesy Mbembe akizungumza kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Manispaa ya Singida wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Afisa Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Singida Babtista Bakasini akizungumza kwenye mkutano huo.
Mmoja wa Wazee wa Manispaa ya Singida akielezea kero yake mbele ya mkuu wa mkoa.
Mkazi wa Manispaa ya Sngida Hadija Ramadhan mkazi wa Unyakhindi akieleza kero yake kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, akizungumza na Mama Amina Ramadhani anayedai mume wake kuuza nyumba kinyemela na kusababisha yeye na watoto kukosa mahali pa kuishi.
Athuman Hassan (maarufu kama GSM) akitoa kero yake kwa mkuu wa mkoa wakati wa mkutano huo.
Mkazi wa Majengo Manispaa ya Singida, Omari Rashid akitoa madai ya baba yake kutekwa na mfanyabiashara mmoja mjini hapa na kupora nyumba yao.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lucas Mwakatundu akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliitaka jamii kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo vya kihalifu.
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Singida wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo.
 

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

MFANYABIASHARA mmoja maarufu wa mjini Singida mkoani hapa anadaiwa kumteka na kumficha kusikojulikana kwa zaidi ya miaka 10 sasa mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wake na haijulikani kama yupo hai au amefariki.

Madai hayo yalitolewa na Omari Rashid juzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika katika viwanja vya  Stendi ya Zamani Manispaa ya Singida.

Rashid ambaye alidai ni mtoto wa mtu huyo aliyetekwa, alieleza kuwa baba yao  hajaonekana tangu mwaka 2010 baada ya mfanyabiashara huyo kumlaghai na kuchukua hati ya nyumba yao na kisha kuwafukuza katika nyumba hiyo ambapo sasa wanaishi kwa kutangatanga.

Aliongeza kuwa mfanyabiashara huyo (anamtaja jina) alimrubuni baba yao kwamba atamlea na familia yake kwa kipindi chote cha maisha yao lakini katika hali ya kushangaza wamejikuta wakitimuliwa na mfanyabiashara huyo ambaye amejimilikisha nyumba yao iliyopo eneo la Majengo Manispaa ya Singida.

Rashid alisema kinachowashanga na kujiuliza maswali yasiyo na majibu ni kwamba baba yao hajaonekana tangu mwaka huo hali inayowafanya waingiwe na hofu kama yupo hai au amekufa.

“Mheshimiwa RC utatusaidiaje jambo hili ili tupate nyumba yetu na tujue hatma ya baba yetu alipo,” alisema.

Kufuatia ombi hilo, Mkuu wa Mkoa Singida, Dk.Mahenge alimwagiza Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida ( DAS) na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lucas Mwakatundu wachukue maelezo ya kina ya mlalamikaji huyo ili serikali iweze kuyafanyia kazi madai yake.

Aidha, Dk.Mahenge aliwagiza viongozi kuanzia ngazi za wilaya hadi chini kujenga tabia ya kuitisha mikutano ya wananchi na kusikiliza kero zao.

 Alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi mafanikio mbalimbali yaliyofanywa na serikali ya awamu sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan  Mkoa wa Singida umepatiwa Sh.Bilioni 230 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, Barabara, Elimu, Umeme na ya Sekta ya Afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here