Home BUSINESS WATAKIWA KUACHA KUFANYA BIASHARA KWA MAZOEA

WATAKIWA KUACHA KUFANYA BIASHARA KWA MAZOEA

 DAR ES SALAAM.

Wanawake wajasiriamali nchini wametakiwa kuacha kufanya biashara kwa mazoea badala yake kurasimisha biashara zao ili kupata fursa mbalimbali za kibiashara.
 
Wito huo umetolewa  tarehe 22 Juni, 2022 na Afisa Sheria kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Vicensia Fuko  wakati akitoa mada kuhusu huduma zinazo tolewa na Wakala katika Mafunzo ya  wanawake wajasiriamali kutoka mikoa  ya Tanzania Bara na Visiwani, yanayofanyika katika ukumbi wa JKT Mgulani Temeke, Jijini Dar es Salaam.

Bi. Fuko amesema wanaporasimisha biashara zao inawapa fursa mbalimbali  za kibiashara ikiwa ni pamoja na kupata mikopo kutoka taasisi za fedha na kushinda zabuni.

“Nichukue fursa hii kuwahamasisha wanawake  wajasiriamali kuhakikisha kuwa mnarasimisha biashara zenu kupitia BRELA  na kwa sasa usajili unafanyika kwa njia ya  mtandao, hivyo hakuna haja ya kufika katika ofisi za BRELA, ” amefafanua Bi. Fuko.


Katika mafunzo hayo ya siku nne, washiriki watajadili masuala mbalimbali yatakayowawezesha kujikwamua kiuchumi sambamba na kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya
 kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, ambao  mwanzilishi wake ni  Mama Anna Mkapa.

Previous articleMFANYABIASHARA SINGIDA ADAIWA KUMTEKA MFANYAKAZI WAKE KWA MIAKA 10 NA KUPORA NYUMBA
Next articleWAUZAJI WA MAGAZETI RUKSA KUFANYA BIASHARA JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here