Home BUSINESS MAVUNDE: MRADI WA SHILINGI BILIONI 500 ZA CHINA KWA ZAO LA SOYA...

MAVUNDE: MRADI WA SHILINGI BILIONI 500 ZA CHINA KWA ZAO LA SOYA KUANZA MWAKA HUU

 Naibu Waziri Kilimo Anthony Mavunde akiongea katika kikao kazi na Washiriki wa mkutano huo na Wawekezaji kutoka China.

Naibu Waziri Kilimo Anthony Mavunde akiwa pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Exaud Kigahe katika kikao kazi na Wawekezaji kutoka China.

 

Mkurugenzi wa Biashara na Fedha Bwana Shangyang Wu kutoka kampuni ya Longping High Tech akiwa pamoja na Mwakilishi wa Longping Tanzania Bi. Juhayna Kusaga pamoja na Washiriki wengine wakimsikiliza Naibu Waziri Mavunde.

  Naibu Waziri Kilimo Anthony Mavunde (Katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Exaud Kigahe, wengine ni Balozi wa Tanzania China, Mbelwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Prof. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Andrew Massawe pamoja na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech leo katika ofisi za Wizara ya Kilimo, Jijini Dodoma.
 
DODOMA.

NNaibu Waziri Kilimo Mhe. Anthony Mavunde leo Juni 2, 2022 ameihakikishia kampuni kubwa ya uzalishaji wa mbegu iitwayo Longping High Tech kuwa Serikali ya awamu ya sita imejipanga kusimaia uwekezaji wenye tija wa zao la soya kuanza mwaka huu ili zao hilo kuanza kuchagia pato la taifa.

Mavunde alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Liang Shi katika kikao kilichohudhuriwa na Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, Balozi wa Tanzania nchini China; Mhe. Mbelwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Prof. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Andrew Massawe. Pia alikuwepo Mkurugenzi wa Biashara na Fedha wa Longping High Tech Bwana Shangyang Wu.

Mavunde amesema Wizara ya Kilimo kwa kutambua umuhimu wa zao hilo katika kuinua maisha ya Watanzania, Wizara imejipanga kuwawezesha watanzania kunufaika na uwekezaji huo huku akiwahakikishia wawekezaji hao kuwa uwekezaji wao utakuwa wenye tija.

Katika kuhakikisha adhma hiyo inatekelezwa, Naibu Waziri Mavunde ataongoza timu ya Wataalam kutoka wizarani na Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara hiyo kwenda mkoani Mbeya kuzungumza na wakulima wa zao hilo ikiwa ni harakati za awali za kuanza kwa uwekezaji huo mkubwa  ambapo uongozi wa Mkoa wa Mbeya umeshatenga ardhi kwa ajili ya zao hilo.

“Hawa Wawekezaji wametembelea sehemu mbalimbali mikoani kuangalia maeneo ya kusaidia uzalishaji wa zao hilo ambapo wamekuwa wakiongozana na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo, na baadhi ya maeneo ambayo wamependa kushirikiana na Wakulima kuendeleza zao hili ni mkoa wa Mbeya ambapo hata Serikali ya mkoa umeshatoa ardhi hekari laki moja wilayani Chunya, ambapo mwekezaji ataliona eneo kabla ya kuanza kwa uwekezaji.” amesema Mavunde.

Mavunde amesema uwekezaji huo, utaongeza tija na uzalishaji wa maharage ya soya kwa sababu, kampuni ya Longping itatoa mbegu bora za soya, zana bora za kilimo kwa Wakulima wa kati na wakubwa na uhakika wa soko baada ya wakulima kuanza kuvuna.

“Wakulima wa Tanzania wamekuwa wakibaliwa na changamoto ya masoko ya uhakika, kwenye uwekezaji huu soko lipo ni kubwa na la uhakika ambapo mkulima ataenda shambani akiwa na uhakika wa wapi atauza mazao yake.”aliongeza Naibu Waziri Mavunde.

Naye Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Wizara yake kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) imejipanga kufanikisha uwekezaji huo.

“Tumeshakubaliana kuwezesha kuanza kwa haraka kwa kwa mradi huu hasa ikizingatiwa kuwa ni matokeao ya mkutano wa Mawaziri wa Afrika, uliofanyika China na na Tanzania ni kati ya nchi tatu za Afrika zilizopata nafasi ya kuuza zao la soya katika soko la China, nchi nyingine ni Benin na Ethiopia.” Amesema Naibu Waziri Kigahe.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amesema kampuni ya Longping inatambulika na imepata baraka zote kutoka serikali ya China na kuzitaka mamlaka zinazohusiana na mradi huu kufanya kazi kwa juhudi kubwa kwa kuwa fursa ya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Sh bilioni 500 itumiwe ipasavyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Andrew Massawe amesema Wizara ya Kilimo itatoa kipaumbele kwa kampuni ya Longping High Tech ili ianze zoezi la kuingiza mbegu bora za soya kwa ajili ya majaribio mapema iwezekanavyo.

“Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI) ipo chini ya Wizara ya Kilimo; Nitahakikisha mnapata ushirikiano wa kutosha, na niseme jambo moja hata kama bado mtakuwa na mahitaji ya ziada msisite kutuambia, ili mpate usaidizi mapema iwezekanavyo”. Alisema Katibu Mkuu Andrew Massawe.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here