Home SPORTS KMC FC WAANZA KUIWINDA SIMBA

KMC FC WAANZA KUIWINDA SIMBA



NA: STELLA KESSY

BAADA ya Jana KMC kutoka sare na Tanzania prisons leo inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo mwingine wa kiporo dhidi ya Simba utakaopigwa siku ya Jumapili ya Juni 19 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Hata hivyo Jana KMC FC iliwakaribisha Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Uhuru mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja ambalo lilifungwa na Matheo Anton.

Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana inaendelea kujifua leo kuzisaka alama tatu nyingine kwenye mchezo huo muhimu ambapo KMC itakuwa ugenini.

Akizungumza na blog hii Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC Christina Mwagala amesema kuwa kikosi chao kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba.

“Tunakwenda kwenye mechi ngumu ambayo kila mmoja anataka matokeo, lakini tunawahakikishia mashabiki zetu kuwa tutaenda kupambana uwanjani kuzisaka alama tatu muhimu”
amesema

“Jana hatujatimiza malengo ambayo tulihitaji kwa maana ya kupata alama tatu, lakini hiyo haitutoi kwenye mapambano , bado tunaendelea kujipanga zaidi kwa michezo inayokuja, tunafahamu kuwa mechi zilizobakia zote ni ngumu lakini tutahakikisha tunashinda.

Hata hivyo kwa upande wa Afya za wachezaji wote wako vizuri na wanahali nzuri ya kujiandaa kwenye mchezo huo dhidi ya Simba hivyo mashabiki na watanzania wote wazidi kuwasapoti kwa kuwa Ligi haijaisha na kwamba watahakikisha Timu inamaliza Ligi kwenye nafasi nzuri.

Hadi sasa KMC imecheza michezo 26 na kukusanya jumla ya alama 32 hivyo kupanda hadi nafasi ya tisa kutoka nafasi ya 10 iliyokuwa kabla ya mchezo wa jana na kwamba imebakiza mechi nne ambazo ni dhidi ya Simba, Mbeya kwanza, Biashara pamoja na Dodoma Jiji

Previous articleTANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KUKUZA TEHAMA
Next articleWAZIRI MCHENGERWA AMPOKEA KIONGOZI WA MABOHORA DUNIANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here