Home LOCAL KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WHO KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA

KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WHO KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA

 

Na:Catherine Sungura,WAF-Dodoma

Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Dkt. Ted Chaiban anatarajia kuja nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Julai 2022

Akizungumza na Waziri wa Afya Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania   Dkt.Zabulon Yoti amesema  kuwa Kiongozi huyo anatarajia kuwasili nchini kwa ziara ya siku nne kuanzia  tarehe 4 hadi 7 mwezi ujao ambapo atapata nafasi ya kutembekea Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Dodoma

Amesema lengo la ziara hiyo hapa nchini ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na masuala mengine ya Afya.

Wizara ya Afya hivi karibuni ilizindua kampeni ya Global Vax Initiatives yenye lengo  la kuhamasisha jamii kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na kufuatilia wale ambao hawakukamilisha chanjo zenye dozi mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here