Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia TAMISEMI Bw. Ramadhan Kailima akichangia hoja katika kikao hicho.
P 3 & 4
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi wakifuatilia kikao hicho.
P 5
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akieleza jambo katika kikao hicho.
P 6
Mjumbe wa Timu ya Uratibu Operesheni Anwani za Makazi Bw. Arnold Mkunde akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni Anwani za Makazi mbele ya kamati hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na:Mwandishi wetu- Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ameongoza kikao cha tisa cha kamati hiyo.
Kikao hicho kimefanyika Juni 02, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali , Wakurugenzi wa Taasisi na wataalamu ambapo wamejadili hatua zilizofikiwa kuhakikisha zoezi la uwekaji wa anwani katika makazi linakamilika kama lilivyokusudiwa.
Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia TAMISEMI Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmmuya, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba na Mratibu Anwani za Makazi Zanzibar Bw. Abdalla Dai Abdalla.
Aidha Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 Agosti 2022 nchini ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10.
MWISHO.