Home SPORTS HABARI PICHA: MATUKIO KUTOKA UWANJA WA MICHEZO WA NKURUNZIZA BURUNDI

HABARI PICHA: MATUKIO KUTOKA UWANJA WA MICHEZO WA NKURUNZIZA BURUNDI

Vijana wa Chipukizi wa Chama cha CNDD-FDD wakionyesha burudani wakati wa ufunguzi wa uwanja mpya wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo katika mkoa wa Makamba nchini Burundi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Ndugu Reverien Ndukiriyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo mkoani Makamba, Burundi.

Pichani baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutoka wilaya ya Buhigwe, Kigoma wakiwa wamejumuika na wenyeji wa Burundi kama Ishara ya Ujirani mwema wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja mpya wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo Makamba nchini Burundi.

Chifu Mtwale Isambe Rugali Buliho wa himaya ya Heru Juu Buha kasulu Kigoma akionyesha uzalendo kwa majirani zake wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex, Makamba nchini Burundi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimvisha medali  kapteni wa timu ya K.C.C.A  ya Uganda John Revita baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya Aigle Noir FC ya Burundi na kuchukua kombe la Nkurunziza Cup, mechi hii imechezwa kwenye uwanja mpya na wa kisasa wa Nkurunziza Peace Park Complex.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here