Home SPORTS VOLLEYBALL WAIWAKILISHA VYEMA NCHIMICHUANI YA KANDA YA TANO BURUNDI.

VOLLEYBALL WAIWAKILISHA VYEMA NCHIMICHUANI YA KANDA YA TANO BURUNDI.

 

Timu za Tanzania mchezo wa Volleball zimeiwakilisha vyema nchi katika michuano ya kufuzu Kanda ya tano Kwa vijana Chini ya miaka 19 (wavulana) na 18 (wasichana) iliyofanyika kuanzia tarehe 10  na kuhitimishwa jana Bujumbura nchini  Burundi.

Katika michuano hiyo Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya pili (2) na ya tatu (3) kutokana na timu mbili za wanaume zilizoiwakilisha nchi na kupewa majina ya Tanzania One (1) na two (2), huku nafasi ya kwanza ikinyakuliwa na mwenyeji Burundi timu ya pili (2)

Michuano hiyo ilihusisha nchi tatu (3) Tanzania, Rwanda na mwenyeji  Burundi ambapo kila nchi ilipaswa kuwakilishwa na timu 4 (2 kila Jinsia) hukuTanzania ikifanikiwa kupeleka timu 2 zote za jinsia moja ya kiume. 

Akizungumzia mashindano hayo kwa simu Katibu Msaidizi na kocha aliyeenda na wachezaji hao Shukuru Ally amewapongeza wachezaji kujitoa kwa kuiwakilisha nchi kwa ushindi huo na kusema kuwa mashindano mengine watajipanga vyema zaidi na watapeleka wachezaji wa jinsia zote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here