Home BUSINESS UNDELEZAJI SEKTA YA VIWANDA UMEENDELEA KUKUA NA KUMILIKIWA KWA SEHEMU KUBWA NA...

UNDELEZAJI SEKTA YA VIWANDA UMEENDELEA KUKUA NA KUMILIKIWA KWA SEHEMU KUBWA NA SEKTA BINAFSI: DKT. KIJAJI

BUNGENI DODMA.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema uwekezaji katika Sekta ya Viwanda umeendelea kukua na kumilikiwa kwa sehemu kubwa na sekta binafsi. 

Pia amesema uwekezaji wa viwanda uko katika Maeneo Maalum ya Uwekezaji (EPZ na SEZ) na maeneo binafsi na viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa hivyo kuongezeka hadi kufika viwanda 541 kutoka viwanda 41 vya sasa. 

Dkt.  Kijaji ameyasema haya wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23 Mei 6, 2022 jatika ujumbi wa Bunge, Dodoma 

Dkt. Kijaji amesema sehemu ya viwanda hivyo ambavyo vimesambaa nchini ni vidogo sana ambavyo ni 62,400 sawa na asilimia 77.07, wakati vidogo ni 17,267 sawa na asilimia 21.33, vya kati ni 684 sawa na asilimia 0.84 na vikubwa ni 618 sawa na asilimia 0.76. 

Alisema kati ya Viwanda Vikubwa 618 ambavyo vimeajiri kuanzia watu 100 ni viwanda 41 pekee vinaajiri zaidi ya watu 500. 

“Viwanda vingi vinajishughulisha na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na vinajielekeza katika kutumia malighafi za ndani kuzalisha bidhaa hizo.” 

Amesema kutokana na usajili wa viwanda chini ya TIC na EPZA, inategemewa kuwa viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa kufikia mwaka 2025 na kufanya idadi ya sasa ya viwanda vikubwa vinavyoajiri wafanyakazi zaidi ya 500 kuongezeka kutoka 41 hadi kufikia 541. 

Dkt. Kijaji amesema tayari Serikali ya Awamu ya Sita imekwishaanza utekelezaji wa Kongani kubwa ya Viwanda ya Kwala ambayo itakuwa na viwanda 200 vikubwa kwa ajili ya kutengeneza nguo, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi, dawa na aina nyingine. 

“Mradi huo umekwishaanza na awamu ya kwanza itakamilika ifikapo mwaka 2024 na viwanda vitatoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000.” 

Amesema uwekezaji katika eneo hilo nakadiriwa kugharimu dola za Marekani bilioni 3 na unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za viwanda katika Soko la Pamoja la Afrika. 

“Viwanda vingine vitatokana na uwekezaji katika Maeneo Maalum ya Nala – Dodoma ambapo tayari Serikali imeanzisha Eneo Maalum la Uwekezaji, pamoja na kongani nyingine kubwa itakayojengwa katika Mkoa wa Mwanza. Uwekezaji huo utafanywa na Serikali ikishirikiana na Sekta Binafsi.” 

“Ni matarajio yetu kuwa, uwekezaji huo utachochea matumizi ya kiuchumi ya miundombinu ya ndani ya nchi hasa Reli ya Kisasa ya SGR, Bandari za Maziwa Makuu, Bahari pamoja na barabara, sambamba na kuongeza wigo wa kodi, kukuza teknolojia na kwa Taifa letu kujitosheleza kwa bidhaa ambazo zimekuwa zikiagizwa kutoka nje ya nchi.” 

Amesema uwekezaji huo utaifanya Tanzania kuwa nguzo ya uchumi ya Bara la Afrika (Africa Economic Power House) ikitumia fursa yake iliyopewa na Mwenyezi Mungu ya kuwa kiunganishi kupitia Bahari – GateWay. 

Kwa upande wa Viwanda Vidogo na vya Kati, Dk Kijaji amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuendeleza mkakati wake wa ujenzi wa viwanda vidogo vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu ili kuzalisha bidhaa ambazo zinaagizwa kwa wingi kutoka nje ilhali zinaweza kutengenezwa hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here