Home Uncategorized SIMBA YALAMBA SUKARI YA KAGERA

SIMBA YALAMBA SUKARI YA KAGERA

 

Na:  Stella Kessy, DAR

MABINGWA watetezi Simba leo wameibuka na ushindi wa  mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo dakika ya 14 Kibu Denic aliipatia timu yake bao la kwanza huku bao la pili limefungwa na John Bocco katika dakika ya 30.

Kwa ushindi huo mpaka sasa Simba imejinyakulia jumla ya alama 49 wakiwa wamepishana alama 8, huku na Kagera Sugar wao wakiwa na nafasi ya 7 na wanajumla ya alama 29.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here