Home LOCAL MOI YAPEWA SIKU 14 KUTENGENEZA MASHINE YA MRI NA CT-SCAN

MOI YAPEWA SIKU 14 KUTENGENEZA MASHINE YA MRI NA CT-SCAN


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dkt Respicious Boniface ndani ya chumba cha mashine ya CT Scan (wa pili ) alipofanya ziara ya kushitukiza leo Mei 11,2022 jijini Dar es Salaam, kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi . PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi (katikati) akizungumza mbele ya Menejimenti ya MOI mara baada kufanya ziara ya kushitukiza leo Mei 11,2022 jijini Dar es Salaam, kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi kwa muda sasa.Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dkt Respicious Boniface na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Tiba (Wizara ya Afya) Dkt Omari Ubuguyu.

 Baaadhi ya Menejiment ya MOI wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo Mei 11,2022 mara baada kufanya ziara ya kushitukiza kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi.Na:Catherine Sungura,WAF-DSM.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amefanya ziara ya kushtukiza Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kukagua mashine za MRI na CT Scan na kubaini zimeharibika.

Hata hivyo, uongozi licha ya kujua hali hiyo haukuwasilisha taarifa rasmi kwa Wizara hiyo, kutokana na hali hiyo Prof. Makubi ameagiza ndani ya siku 14 kuanzia sasa wahakikishe mashine hizo zilizonunuliwa kwa gharama kubwa na Serikali, zitengenezwe na kuanza kutoa huduma.

Prof. Makubi ameziagiza hospitali za Rufaa za Mikoa, Kanda na Taifa kuwa na mpango mbadala (Plan B) kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kupata matibabu bila usumbufu pale mashine za Taasisi zao zinapoharibika.

“Kwa mfano hapa MOI (Plan B) yenu ni Muhimbili, wagonjwa ambao wanahitaji CT Scan na MRI wapate huduma bila kupata usumbufu na rafiki” ameagiza.

Aidha, ameziagiza ziwe na ‘plan B’ kwa vipimo vyote vya radiolojia na vipimo vya damu endapo itatokea changamoto wagonjwa waendelee kupata huduma.

Ameelekeza pia hospitali zote za Taifa, Kanda, Mikoa na maalum zenye mashine za kisasa kuhakikisha zinatenga asilimia kadhaa ya fedha kwa ajili ya matengenezo yake kutoka kwenye makusanyo ya ndani

Hata hivyo ameelekeza tena hospitali zote hizo kukaa na TANESCO na kufanya tathmini ya mifumo ya umeme lakini pia ziweke ‘backup’ ya nishati mbadala ili mifumo hiyo isiharibike pale inapotokea kukatika kwa umeme.

Vilevile amewlekeza pia kutengwa bajeti mahususi ya matengenezo na kutoa miezi mitatu (3) kuwa na mkataba wa matengenezo kwa mashine zote pamoja na vifaa vya maabara kwa hospitali zote za Rufaa za Mikoa,Kanda,Maalumu ma Taifa ili kuhakikisha zinafanyiwa matengenezo na ukarabati kwa wakati.

 
Previous articleSIMBA YALAMBA SUKARI YA KAGERA
Next articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 12-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here