Home LOCAL SERIKALI IMEZINDUA MWONGOZO KWA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHITAKA WA KESI ZA RUSHWA

SERIKALI IMEZINDUA MWONGOZO KWA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHITAKA WA KESI ZA RUSHWA

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Godfrey Pinda (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi Mwongozo wa Kiutendaji wa Upelelezi na Uendeshaji wa Mashtaka wa Kesi za Rushwa, uzinduzi huo umefanyika leoMei 31,2022 Jijini Dar es Salaa. (kushoto) ni DPP Sylivester Mwakitalu.

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Godfrey Pinda akizungumza na wadau mbalimbali katika uzinduzi huo muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi muongozo huo.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali DPP Sylivester Mwakitalu akizungumzia Mwaongozo huo alipokuwa akimkaribisha Mgeni rasmi katika hafla hiyo.





Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Wizara ya sheria na Katika imezindua Mwongozo wa Kiutendaji wa Upelelezi na Uendeshaji wa Mashtaka wa Kesi za Rushwa ambao umetolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka chini ya kifungu cha 18 na 24 vya Sheria ya Usimamizi wa Mashtaka, Sura ya 430 nchini.

Akizindua Mwongozo huo amefanyika leo Mei 31,2022 Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya waziri, Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu  Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Geoffrey Mizengo Pinda (Mb) amesema kuwa, Serikali kupitia wizara hiyo itashirikana kwa karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kuhakikisha mfumo bora wa utoaji haki kwa wananchi inazidi kuimarika na kuleta ufanisi.
 
“Lazima tuziimarishe moja wapo ni kitengo hiki cha DPP, kwa Mwanasheria Mkuu, lakini tumeenda mbali zaidi lazima tufanye kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na kule tuna play part kubwa sana tunazo magereza zetu zinatakiwa kuimarishwa,”amesema Mheshimiwa Geophrey Pinda na kuongeza,

“Na nyie Mahakama ile huduma ambayo mmeanza kutoa lazima iwe connected na nyie kwa maana ya Video Conference Programs ambazo zinaendelea upande wa Mahakama kwa kusikiliza kesi zikiwa mbali kwa hiyo lazima tujenge uwezo tushirikiane na idara ya polisi kwa maana ya Wizara ya Mambo ya Ndani tuweze kuhakikisha kwamba huduma zinaimarishwa maeneo yote ya utoaji haki, sasa hata tukijiimarisha sisi Wizara ya Katiba na Sheria tukawaacha wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Ndani bado tunakuwa hatujafikia lile lengo ambalo ndilo lengo kuu kabisa,”amesema Mheshimiwa Pinda.

Ameongeza kuwa, dhamira ya Serikali ni kuendelea kuwa na mfumo mzuri wa utoaji haki kwa wananchi hivyo ushirikiano wa dhati wa wizara hizo ni muhimu sana kuwezesha wananchi kupata haki zao pamoja na kuendesha shughuli za maendeleo kwa ufanisi.
 
“Niwaombe tuwe na ushirikiano wa kutosha na pale sisi ni wasemaji wenu kwa maana ya Serikali, ninyi hamna majukwaa ya kusemea sisi ndio tunasema tukikaa kwenye eneo. Tushirikishwe kwa asilimia zote ili tujenge mfumo bora na tujenge mfumo bora wenye matokeo makubwa badala ya kuacha tusishirikiane,”amesema.

Na kuongeza kuwa “tumepambana sana kujengea uwezo DPPOs hela iliyoongezeka haikuwa lengo letu, tuliomba hela nyingi, lakini kutokana na uwezo wa Serikali wametuhold kidogo tunasubiri subiri, lakini matarajio yetu ni kwamba lazima tuwajengee uwezo ili muweze kufika kila kona zote za nchi muwe na ofisi mahali pote, lakini vitendea kazi kuna wilaya hazijafikia na huduma zenu tunahitaji mtoke wilaya moja muende kuhudumia wilaya zingine…ili muende sambamba na mabadiliko,”amesema Mheshimiwa Pinda.
 
Kwa upande wake Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, DPP Sylivester Mwakitalu amewapongeza wadau wa maendelo ikiwemo Serikali ya Uingereza na Umoja wa Ulaya ambao wameshiriki kikamilifu kufanikisha juhudi mbalimbali za Serikali katika kupambana na vitendo vya rushwa.

Aidha DPP Mwakitali amesema kuwa, upelelezi wa makosa ya rushwa unahitaji umakini wa hali ya juu kutokana na makosa hayo kufanywa na watu wenye weledi, hivyo upelelezi wake unahitaji umakini na umahiri ndiyo maana Ofisi ya Taifa ya Mashitaka kwa kushirikiana na wadau waliona ni vyema wakatengeneza mwongozo huo ambao utawasaidia wapelelezi na waendesha mashitaka wanapoendesha kesi hizo ili kuleta usawa.

 
“Mwongozo huu utawawezesha wapelelezi na waendesha mashitaka kushughulikia kesi za rushwa kwa urahisi na tija. Baada ya kuzinduliwa utasambazwa na kuhakikisha kwamba watendaji wote wanaupata na pale itakapolazimika kufanya mafunzo ili kurahisisha wauelewe na wautumie kikamilifu.Mwongozo huu ni nyenzo muhimu sana utatusaidia kupata matokeo chanya katika kupambana na rushwa,”amesema DPP Mwakitalu.

Kwa upande wao wawakilishi wa mabalozi, Bw.Simon Charter kwa niaba ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania na Simon Van Broek kwa niaba ya Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania wamesema kuwa, wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kupambana na vitendo vya rushwa.

Sambamba na shughuli mbalimbali za maendeleo Ili iweze kutekeleza kikamilifu miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here