Home LOCAL RC MAKALLA AWATAKA WAAJIRI KUWASILISHA MICHANGO YA WAFANYAKAZI KWA WAKATI

RC MAKALLA AWATAKA WAAJIRI KUWASILISHA MICHANGO YA WAFANYAKAZI KWA WAKATI

– Ataka Maafisa kazi kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara.

– Awashukuru Wafanyakazi kwa ushirikiano na kuendelea kufanya Kazi.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ameongoza Maelfu ya Wafanyakazi wa Mkoa huo kwenye Sherehe za Mei Mosi ambapo amewapongeza Wafanyakazi kwa utendaji mzuri katika kuchochea Uchumi na utoaji wa huduma Bora kwa jamii.

RC Makalla amesema miongoni mwa Mambo anayojivunia kwa Wafanyakazi wa Mkoa huo ni Ongezeko la mapato, huduma Bora za Afya, Maji, Ufaulu mzuri mashuleni na miradi ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa mahadhimisho hayo ambayo kimkoa amefanyika Uwanja vya Uhuru, RC Makalla amewataka Waajiri wote kuwasilisha michango ya Wafanyakazi kwa wakati katika mifuko ya hifdhi ya jamii.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi, na Waajiri kulipa fedha za uhamisho na madai mbalimbali ya Wafanyakazi.

Katika Sherehe hizo, RC Makalla amepokea Maoni na mapendekezo ya Wafanyakazi kupitia hotuba ya Wafanyakazi wa Mkoa huo ambapo ameahidi kupatia ufumbuzi changamoto zilizo ndani ya uwezo wake na zile zinazohitaji kutatuliwa na Mamlaka za juu ataziwasilisha.

Hata hivyo RC Makalla amesema amewataka Wafanyakazi kuendelea na kazi wakati changamoto walizowasilisha zinaendelea kufanyiwa kazi na Serikali sikivu ya awamu ya sita.

Mahadhimisho ya Mei Mosi kwa Mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu isemayo “Mishahara na maslahi Bora ya Wafanyakazi, Kazi IENDELEEE”.

Previous articleBRELA YASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI DAR
Next articleSTAMICO YASHEREHEKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here