Home LOCAL RC GEITA ACHARUKA UJENZI WA VETA ATOA SIKU 30 KUKAMILIKA.

RC GEITA ACHARUKA UJENZI WA VETA ATOA SIKU 30 KUKAMILIKA.

 Na:Costantine James, Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Rosemary Senyamule amemtaka mkandarasi anaejenga chuo cha ufundi stadi (VETA) kukamilisha haraka ujenzi wa chuo hicho ili kianze  kutoa elimu kwa viajana.

Amesema hayo wakati alipofanya ziara  katika eneo ambapo kinajengwa chuo hicho yenye lengo la kukagua mwenendo wa ujenzi wa Chuo cha VETA kinachojengwa katika halmashauri ya mji Geita mkoani Geita.

Senyamule  amesema hajalidhishwa na mwenendo wa ujenzi hivyo amemuagiza Mkandarasi anaesimamia ujenzi huo kuhakikisha anasimamia kikamilifu ili ifikapo juni 20 awe amekamilisha ujenzi huo.

Wakati akikagua ujenzi wa chuo hicho Senyamule amesema mradi huo ulisimama kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na mapungufu ya mkandarasi na sasa unajegwa kwa force account chini ya usimamizi wa mhandisi mshauri toka chuo cha ufundi Arusha.

Mhe, Senyamule amesema serikali chuni ya Rais Samia suluhu Hassani imeamua kuwekeza kwa vijana katika upande wa elimu ili vijana nchini wapate elimu ya ufundi katika Nyanja mbalimbali hali itakayowawezesha kuijiajiri.

Mhandisi John Idelya ambae ni msimamizi wa ujenzi wa chuo cha VETA mkoa wa Geita amesema mpaka sasa ujenzi wa chuo hicho umefikia asilimia 51% huku akisema sababu zilizopelekea kuchelewa kwa kukamilika kwa mradi huo ni hali ya mbaya ya  hewa.

Mhandisi John amesema ujenzi wa Chuo hicho utagalimu kiasi cha bilioni 4.4 mpaka kukamilika kwake hata hivyo amemuhakikishia mkuu wa mkoa Geita Mhe, Rosemary Senyamule kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo ifikapo juni 20 2022.

Amesema atahakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi wa chuo hicho kwa kufanya kazi usiku na mchana pamoja na kuongeza idadi ya mafundi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya mda uliopangwa.

Kwa upande wake afisa elimu watu wazima mkoa wa Geita Salome Cherehani amemtaka mkandarasi anaesimamia ujenzi huo kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kutoa taarifa juu ya mwenendo wa ujenzi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.

Ujenzi wa Chuo hicho utakapokamilika utakuwa na idadi ya majengo 26 yakiwemo madarasa ya kusomea pamoja na karakana mbali mbali zitakazotumika kujifunzia fani ya umeme, utengenezaji wa magari, mabweni ya wanafunzi, na majengo ya utawala.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here