Home LOCAL MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO ILALA MEI 12

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO ILALA MEI 12

Na: Heri Shaaban

MWENGE wa Uhuru  unatarajia kuzindua miradi ya maendeleo iliyopo Wilaya ya Ilala Mei 12 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari Wilayani Ilala Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija, alisema Mwenge wa Uhuru unatarajia kupokelewa Kinyerezi Mtaa Kifuru Jimbo la SEGEREA.

Ludigija alisema siku ya Mei 12 Mwenge utakapowasili Ilala unatajia kupokelewa saa kumi na mbili ASUBUHI Kata ya  Kinyerezi .

Ng’wilabuzu  LUDIGIJA amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge siku hiyo.

Mkuu wa Wilaya llala Ng’wilabuzu alisema Mwenge huo mara baada kuwasili Ilala unatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi ya Afya , Barabara,vikundi vya kijamii na Lishe.

Alisema mara baada kuwasili Ilala na kuzindua miradi ya Maendeleo Mwenge huo unatarajia kulala Jimbo la Ukonga eneo la Ukonga Mzambalauni Shule ya Msingi ambapo Burudani mbalimbali mziki wa KIZAZI  kipya zitakuwepo ..

Akizungumzia sehemu ambayo inalala Mwenge alisema pia kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali pamoja na upimaji Afya VVu UKIMWI na  Chanjo ya UVIKO 19.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here