Home BUSINESS BRELA YAWATAKA WAJASIRIAMALI VIZIWI KURASIMISHA BIASHARA

BRELA YAWATAKA WAJASIRIAMALI VIZIWI KURASIMISHA BIASHARA

DAR ES SALAAM.

Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali  viziwi kurasimisha biashara zao ili kukidhi takwa la kisheria. 

Wito huo umetolewa  Mei  05, 2022 na maafisa wa BRELA katika warsha  iliyoandaliwa maalum kwa wajasiriamali viziwi kutoka wilaya ya Temeke  iliyofanyika ukumbi wa Mbagala Spiritual Center  jijini Dar es salaam.

Akiwasilisha mada kuhusu usajili wa majina ya biashara na makampuni,  Afisa Usajili wa BRELA Bw. Englibert Barnabas,  ameeleza kuwa ni muhimu kwa kila mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake kwani vigezo katika usajili ni vichache na itarahishisha wao kutambulika kwa wateja wao na kukuza soko la bidhaa wanazozizalisha na kuuza.

Ameongeza kuwa ili msajili aweze  kukubali kusajili jina la biashara ni lazima liwe la kipekee na lisifanane na jina jingine.

Aidha amewataka wadau kutembelea mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao  wa (ORS)  ili kurasimisha biashara zao, na hatimaye kunufaika na fursa mbalimbali zinazojitokeza.

Kwa upande wake Msadizi wa usajili kutoka BRELA, Bi. Yvonne Masele amesisitiza umuhimu wa   kusajili alama za bishara na huduma kwani kwa kufanya hivyo kunatoa wigo wa kuendelea kiuchumi na kukuza soko na huduma.

Nae Bw. Rajab Chambega. Afisa Leseni kutoka BRELA ameelekeza namna bora  ya utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda na manufaa yake kwa ujumla.

Bw. Chambega amesema BRELA ipo bega kwa bega na wadau wote ili kuhakikisha elimu hiyo inamfikia kila mmoja huku akiwataka maafisa biashara katika halmashauri husika kuwa msaada  na daraja kwa wadau ili kupata elimu ya urasimishaji wa biashara zao.

Nao washiriki wa warsha hiyo wameeleza kuridhishwa na elimu waliyoipata katika warsha hiyo ,  huku wakiahidi kuwa mabalozi  katika ufikishaji wa taarifa juu ya namna bora ya urasimishaji wa biashara, kwa jamii inayowazunguka.

BRELA imedhamini na kutoa mafunzo wa wajasiriamali viziwi lengo likiwa ni kuwajengea uwezo juu ya urasimishaji wa biashara.

Previous articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 6-2022
Next articleMWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO ILALA MEI 12
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here