Home ENTERTAINMENTS MBUNIFU NEAH COLLECTION ATUA MISS TANZANIA 2022

MBUNIFU NEAH COLLECTION ATUA MISS TANZANIA 2022

NA:  MWANDISHI WETU

MBUNIFU nyota wa mavazi nchin Neah Pipo ‘Neah Collection’, ameishukuru kamati ya Miss Tanzania 2022, kwa kumpatiq frusa ya kubuni nguo za washiriki katika vazi la opening dance.

Neah ni miongoni mwa wanamitiando kutoka mkoa wa Tanga, ambao wamekua wakidhamini mashindano ya urembo hapa nchi miongoni mwao ni Miss pwani 2021 na Miss Tanga 2021.

Akizungumza na ukurasa huu amesema anapenda kudhamini mashindano hayo kwa sababu yeye ni mmoja wa vijana wa kike ambao wanapenda kuibua vijana wenye vipaji.

“Mashindano ya urembo yamekua chachu ya kuibua vipaji vya wasichana ambavyo vimeleta maendeleo kwa jamii hivyo mimi kama mbunifu wa mavazi nchin nimeamua kutumia kipaji changu kuinua mabinti hawa,” anasema Neah Collection.

Mbali na kudhamini mashindano ya urembo amekuwa akishiriki kuonyesha mavazi katika matamasha tofauti hapa nchini ikiwemoa Swahili Fashion Week, Tanzania Fashion Festival, Runway Bay na Leady in Red.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here