Home LOCAL MBUNGE BONAH AFANYA ZIARA KWENYE BARABARA YA CHANG’OMBE-MACHIMBO

MBUNGE BONAH AFANYA ZIARA KWENYE BARABARA YA CHANG’OMBE-MACHIMBO

NA:  HERI SHABAN(SEGEREA).

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah  Kamoli, amesema SERIKALI inatarajia kujenga Barabara za kisasa katika mradi wa kuboresha Miundombinu  ya jiji la Dar Salaam (DMDP) katika mwaka wa FEDHA 2022 /2023

Mbunge Bonah  aliyasema hayo katika ziara yake Jimboni Segerea kutatua kero za wananchi Segerea na Kinyerezi leo.

“Katika kikao cha Bajeti kinachoendelea Dodoma nilielezea suala la Barabara zilivyo kero Jimbo la Segerea ,Bajeti ya Mwaka wa fedha 2022 /2023 ambayo inaanza mwezi June mwaka huu barabara za Kata ya Segerea zilizopo katika Mradi wa DMDP zitaanza kujengwa kwa kiwango Cha lami Pamoja na Taa za Barabarani” alisema Bonah.

Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli alitaja moja ya Barabara korofi  ambayo ipo katika Mradi wa DMDP  ni Chang’ombe – Kundy -Mbuyuni nayo ipo kwenye mpango huo kama ilivyo ainishwa kwenye mapendekezo na Diwani wa Kata hiyo na Diwani  Robert Manangwa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya SEGEREA  Robert Manangwa alisema Barabara ya Changombe kwa -Kundy -Machimbo hadi Mbuyuni  ipo kwenye mipango ya kutengenezwa kwa kiwango cha lami lakini wakati tunaendelea kusubiri budget hiyo ,Tayari wameianisha kwenye budget ya Tarura ili iendelee kukarabatiwa kuondoa usumbufu kwa wananchi.

DIWANI ROBERT MANANGWA aliongeza kwa kusema “Mkandarasi ambaye atapangiwa Barabara hiyo ni vyema akaangalia maeneo korofi ili wayatengeneze vizuri kuondoa usumbufu kwa wananchi”

Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Ilala Joseph Sililo alisema tenda ya Barabara kwa ajili ya matengezo ya Barabara hiyo na nyingine ambazo ziko kwenye mpango wa TARURA Wilaya ya Ilala wameshatangaza kuanzia leo kwenye  mfumo na kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Saba ukarabati utaanza mara moja!!

Mwisho.

Previous articleSHAKA ATAKA WANANCHI WAPEWE NAFASI KUSHUHUDIA UTEKELEZAJI WA MIRADI.
Next articleWACHIMBAJI WA MADINI MKOANI GEITA WATAKIWA KUTUMIA VIFAA VYA USALAMA KAZINI ILI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA MAGOJWA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here