Home BUSINESS MANDALIZI MKUTANO WA 65 UNWTO-CAF YAANZA, DKT MICHAEL ASISITIZA WANAKAMATI...

MANDALIZI MKUTANO WA 65 UNWTO-CAF YAANZA, DKT MICHAEL ASISITIZA WANAKAMATI KUCHUKULIA UMUHIMU NA UZITO JUKUMU WALILONALO


katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dkt Fransis Michael akiongea katika kikao Cha kwanza Cha kamati kuu ya maandalizi ya mkutano wa 65 wa shirika la utalii Duniani- kamisheni ya Afrika.

katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dkt Fransis Michael akikabidhi nyaraka za maandalizi ya mkutano wa UNWTO-CAF kwa wenyeviti wa kamati kama ishara ya kuzindua kamati kamati hiyo.


Picha ya pamoja za wajumbe wa kamati kuu ya maandalizi ya mkutano wa 65 wa shirika la utalii Duniani-kamisheni ya Afrika (UNWTO-CAF)

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Maandalizi ya mkutano wa 65 wa shirika la utalii Duniani- kamisheni  ya Afrika (65 UNWTO-CAF) yameanza rasmi ambapo katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dkt Fransis Michael amezindua kamati ya maandalizi huku akiwasisitiza kuchukulia umuhimu na uzito jukumu walilonalo.

Dkt Fransis alisema kuwa wanasababu zote za kujivunia Tanzania kupata fursa ya kuandaa mkutano huo utakaofanyika tarehe 5 ha7 October ambao pia utatoa fursa ya kuitangaza nchi kwani utaleta watu wengi ambao watakuja kushuhudia yale yaliyotangwaza na Rais Samia Suluhu katika filamu ya Royal Tour hivyo ni vema wanakamati  wakapangilia mambo yote mapema.

“Tumejaribu kutafuta watu kutoka katika nyanja, wizara zote katika kamati hii ili kusudi tuweze kuhakikisha kwamba maandalizi haya yanakuwa bora na yanafana na kuweza kufanya mkutano huu kuwa wa mfano,”Alisema Dkt Fransis.

Alifafanua kuwa majukumu makubwa ya kamati hiyo ni kuandaa mkutano ambapo wanatakiwa kuandaa uweze kufana na kuwa kivutio kikubwa Kuvutia watu wa nje na mataifa mengine kuja kutembelea nchi ya Tanzania.

“Tunatakiwa tuhakikishe kuwa kamati inafanya kazi kwa weledi kwasababu mkutano huu ni wa kimataifa, tunaleta viongozi wa nchi na nchi zingine hivyo ni lazima tuhakikishe Tanzania tunakuwa mfano wa nchi zingine,”Alieleza.

Kwa upande wake Felex John mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo kutoka Tanzania bara ambaye pia ni kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii  alisema kuwa tukio hilo wanalichukulia kimkakati kwasababu ni tukio ambalo linakwenda kuleta wageni wengi katika nchi.

“Ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo wa mkakati wetu wa utalii mikutano ambao unalenga watalii wengi na wegeni kuja katika nchi yetu kwahiyo kama mnavyofahamu mkutano huu utakunisha mawaziri wanaosemamia sekta ya utalii na uhifadhi kutoka nchi zote barani Afrika lakini pia watakuja na watu wengi hivyo wadau wetu muhimu wa sekta ya utalii wajiandae kupokea idadi kubwa ya wageni kutoka mataifa yetu ya Afrika,” Alisema Felex John.

Naye mwenyekiti mwenza kutoka Tanzania Zanzibar Rahim Bhaloo alisema kuwa Tanzania imejifungua katika sekata ya utalii, Rais Samia Suluhu ameitangaza sana vivyo hivyo na Rais Hussein Mwinyi ambapo ni fursa kwa Tanzania kujiuza kwa dunia  kwa kujitangaza na  kuonesha vivutio.

“Ni muda wa kuamka na ni lazima washirikiane wote kwa pamoja kwani hizi ni fursa ambazo zitakuwa na fursa kwa watanzania hasa wananchi wa chini ambao wapo moja kwa moja katika sekta ya utalii hivyo waitumie fursa hiyo kujiletea maendeleo kama nchi na kama watanzania,” alisema Bhaloo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here