Hayo yamebainisha leo katika mkutano baina ya Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na Rais wa Taasisi hiyo Prof. Chang-Yup Kim
Waziri Ummy amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikichangia vipaumbele vya sekta ya afya toka mwaka 2006 ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma pamoja na kuwajengea uwezo wataalam wa afya.
Katika mkutano huo Waziri Ummy ametumia mkutano huo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea pamoja na Taasisi ya KOFIH kwa misaada yao wanayoendelea kuitoa ikiwemo uimarishaji wa huduma katika hosoitali ya Mloganzila pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ( Tumbi).
Vilevile, Waziri Ummy ameiomba KOFIH kutoa mchango katika eneo la Afya ya Mama na Mtoto kwa lengo la kupunguza vifo katika kundi hilo.
Kwa upande wake, Rais wa Taasisi ya KOFIH amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Korea ya Kusini hususani uwepo wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini ambao kwa kiasi kikubwa umechagiza na kuimarisha uhusiano zaidi.
Rais huyo wa KOFIH anatarajia kufanya ziara katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania mwezi Juni, 2022 kwa lengo la kuendeleza majadiliano maeneo yatakayofadhiliwa katika mzunguko ujao wa misaada ya Taasisi hiyo.