Home LOCAL KOFIH YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUIMARISHA UTOAJI WA...

KOFIH YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Taasisi ya Korea Foundation for Internation Health Care(KOFIH) imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya.

Hayo yamebainisha leo katika mkutano baina ya Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na Rais wa Taasisi hiyo Prof. Chang-Yup Kim 

Waziri Ummy amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikichangia vipaumbele vya sekta ya afya toka mwaka 2006  ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma pamoja na kuwajengea uwezo wataalam wa afya. 

Katika mkutano huo Waziri Ummy ametumia mkutano huo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea pamoja na Taasisi ya KOFIH kwa misaada yao wanayoendelea kuitoa ikiwemo uimarishaji wa huduma katika hosoitali  ya Mloganzila pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ( Tumbi).

Vilevile, Waziri Ummy ameiomba KOFIH kutoa mchango katika eneo la  Afya ya Mama na Mtoto kwa lengo la kupunguza vifo katika kundi hilo. 

Aidha, ameiomba KOFIH itoe msaada katika kufadhili kwa wataalam wa maabara, wahandisi na wateknolojia wa vifaa tiba na wauguzi ili waweze kutoa huduma za afya zenye ubora. 

Kwa upande wake, Rais wa Taasisi ya KOFIH amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Korea ya Kusini hususani uwepo wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini ambao kwa kiasi kikubwa umechagiza na kuimarisha uhusiano zaidi. 

Rais huyo wa KOFIH anatarajia kufanya ziara katika nchi za Afrika  Mashariki ikiwemo Tanzania mwezi Juni, 2022 kwa lengo la kuendeleza majadiliano maeneo yatakayofadhiliwa katika mzunguko ujao wa misaada ya Taasisi hiyo.

Previous articleKANUNI MPYA ZA MAFAO YA PENSHENI YATANGAZWA RASMI KUFUATIA AGIZO LA LA RAIS SAMIA
Next articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 27-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here