Home LOCAL JENGO LA HUDUMA ZA DHARURA TABORA LAKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA JUMATATU

JENGO LA HUDUMA ZA DHARURA TABORA LAKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA JUMATATU

Tabora.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof.Abel Makubi leo ametembelea utekelezaji wa ujenzi wa jengo la huduma za dharura na wagonjwa mahututi katika hospitali ya rufaa ya Kitete-Tabora ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 100 na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 604.

Prof.Makubi amesema kuwa jengo hilo la huduma za dharura litakua na vitanda 28 na litakua na uwezo wa kuwahuduma wagonjwa wengi wa dharura wa ajali mara moja kwa mpigo.

#AfyaKwanza
#JaliAfyaYako

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here