Home BUSINESS HABARI PICHA: KIKAO KAZI KATI YA BRELA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA...

HABARI PICHA: KIKAO KAZI KATI YA BRELA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI CHAMALIZIKA MKOANI MOROGORO


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Seka Kasera akizungumza alipokuwa akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa (BRLA) Godfrey Nyaisa alipokuwa akifunga rasmi Kikao kazi cha siku mbili kati ya BRELA na Wahariri wa Vyombo vya Habari kilichokuwa kikifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mei 21, hadi 22, 2022 Mkoani Morogoro.


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma wa BRELA Bi. Rhoida Andusamile akiongoza Majadiliano ya Mkakati wa Ushirikiano kati ya BRELA na Vyombo vya Habari wakati wa Kikao kazi kati ya wahariri wa vyombo vya Habari na BRELA kilichofanyika kwa siku mbili Mei 21 na 22, 2022 Mkoani Morogoro.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara wa BRELA Meinrad Rweyemamu akitoa mada kuelezea Majukumu ya Kurugenzi ya Makampuni na Majina ya Biashara, Mafanikio na Maboresho kwenye masuala, katika kikao kazi cha siku mbili kati ya wahariri wa vyombo vya habari na BRELA leo Mei 22, 2022 Mkoani Morogoro.


Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Bunifu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Seka Kasera akionesha Bidhaa alipokuwa akitoa mada ya miliki Bunifu na alama za Biashara katika Kikao kazi hicho Mkoani Morogoro.
 


Mkurugenzi wa Leseni wa BRELA Andrew Mkapa akitoa mada kuhusu utoaji wa Leseni katika kikao kazi hicho Mjini Mrogoro.
 

Afisa habari Mkuu wa BRELA Theresa Chilambo (kulia) akiwa na Mhariri wa Gazeti la habari leo Mgaya Kingoba (katikati) pamoja na Mhariri wa Gazeti la Nipashe Joseph Mwendapole (kushoto) wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara Meinrad Rweyemamu (hayumo pichani) kwenye kikao kazi hicho leo Mei, 22,2022 Mjini Morogoro.
Wahariri waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara Meinrad Rweyemamu (hayumo pichani) kwenye kikao kazi hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mhariri wa Clouds Media Group Joyce Shebe (kushoto) akiwa na Mhariri Mwandamizi wa maudhui ya Mtandaoni (AZAM MEDA) Jennifer Sumi (kulia) wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Mhariri Mwandamizi wa habari wa AZAM TV Samson Mfalila (kulia) akiwa na mhariri wa Maudhui ya Mtandaoni wa AZAM Media Jennifer Sumi (katikati) na Mhariri wa Clouds Media Joyce Shebe (kushoto) wakisikiliza mada kutoka kwa muwasilishaji Meinrad Rweyemamu Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara BRELA (hayumo pichani) leo Mei 22,2022 ikiwa ni siku ya mwisho ya Kikao kazi cha siku mbili Mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile akifuatilia kwa makini Kikao kazi hicho leo Mei 22,2022 Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Fullshangwe Blog John Bukuku akiwa katika kikao kazi hicho leo Mei 22,2022 Mjini Morogoro.


Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anitha Mendoza (kushoto) akiwa na Mwanachama wa Jukwaa hilo Apolinary Tairo (kulia) katika Kikao kazi hicho.


Mhariri wa Michuzi Media, Michuzi JR (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Diramakini Blog Godfrey Nko (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Fullshangwe Blog John Bukuku wakiwa kwenye kikao kazi hicho Morogoro.

Nevile Meena Mjumbe wa Kamati ya utendaji wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), (kulia) akijadiliana jambo na Mhariri wa Upendo Radio ya Jijini Dar es Salaam, na Mwanachama wa (TEF) Upendo Urembo (kushoto) katika kikao kazi hicho.

PICHA ZA WAHARIRI MBALIMBALI WAKIWA KWENYE KIKAO KAZI HICHO.

Previous articleVideo Mpya : BBY NAI – NIMEOLEWA…NI YULE MREMBO ALIYETEMBEA MTAANI NA BANGO LA ‘NATAFUTA MME’
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JUMATATU MEI 23-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here