Home LOCAL CCM YAWAKILISHA MAONI YAKE KWA KIKOSI KAZI

CCM YAWAKILISHA MAONI YAKE KWA KIKOSI KAZI

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amewasilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi kwa Kikosi Kazi Cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachofanyia kazi masuala yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa leo tarehe 24, Mei 2022 jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho cha kuwakilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu Chongolo aliongozana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here