Home LOCAL CAG AWATAKA WAHARIRI KUJIIMARISHA KATIKA HABARI ZA UCHUNGUZI

CAG AWATAKA WAHARIRI KUJIIMARISHA KATIKA HABARI ZA UCHUNGUZI


Mkaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) CPA Charles Kichere akizungumza alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi katika kikao maalum kati ya Ofisi yake na waariri wa vyombo vya habari kilichofanyika Mei 28,2022 Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa TEF Deodatus balile akimsikiliza CAG Kichere (hayumo pichani) kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungmza katika mkutano huo mara baada ya CAG kuwasilisha mada kwa Wahariri hao Mei 28,2022.


Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akifuatilia michango ya Wahariri wa Habari (hawamo pichani) walipokuwa wakizungumza na kuuliza maswali.kwenye mkutano huo.


DAR ES SALAAM.

Wahariri wa Habari nchini wametakiwa kujikita na kujiimarisha katika kuandika habari za uchunguzi (Investigative Journalism) ili kuwezesha kulinda rasilimali za umma kwa manufaa ya nchi.  

Hayo yamesemwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere katikamevitaka vyombo vya habari nchini kujikita

Amesema,  vipo vyombo vya habari vichache hasa magazeti ambayo yamejikita kuandika habari za uchunguzi na kwamba yanafanya vizuri sana katika kuandika habari za uchunguzi ambazo zina tija  kwa taifa.

Ameyasema hayo Mei 28,2022 wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa Wahariri wa vyombo mbalimbli jijini Dar es Saalaam ambapo pamoja na mambo mengine amevipongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kufanya kazi nzuri kwa kutumia kalamu zao kufikisha habari za  ripoti za ukaguzi kwa wananchi na wadau wengine.

“Vyombo vya habari yakiwemo magazeti, radio, televisheni, mitandao ya kijamii na kadhalika vimekuwa vikiwafahamisha wananchi kwa mapana na marefu juu ya yaliyomo kwenye ripoti hizo mara baada ya kuwasilishwa bungeni. Kwa kweli ushirikiano wenu umekuwa ni chachu ya ripoti za CAG kufahamika kwa wananchi na wadau wengine majukumu mliyobeba yana thamani sana kwetu na tunawashukuru sana kwa hilo, amesema CAG Kichere.

Ameongeza kuwa, kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari ameamua kukutana na Wahariri wa ili kuwafafanulia masuala mbalimbali yanayohusiana na ukaguzi katika kuwajengea uelewa mpana zaidi  wa kutambua mambo mbalimbali na shughuli zinazofanywa na Ofisi ya CAG, majukumu yake kikatiba, mamlaka pamoja na ripoti wanazozitoa.

Ni katika kuchagiza mahitaji ya uwazi na uwajibikaji katika shughuli za Serikali katika kuelimisha jamii juu ya masuala ambayo yana tija kwa nchi yetu. Hivyo huu si mkutano wa kawaida bali ni mkutano wenye lengo  mahususi la kuwajengea uwezo ninyi Wahariri wa vyombo vya habari kuwa na uelewa juu mamlaka niliyonayo, majukumu niliyopewa kikatiba pamoja na ripoti mnazotoa.

“Mihimili mitatu ya dola ambayo inamajukumu yake mahususi kwa kila mhimili kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na sheria zetu tulizonazo.Lakini kama ambavyo imekuwa imesemwa na kufahamika kwa wengi vyombo vya habari ni mhimili  usio rasmi na unaitwa mhimili wa nne,” amesema.

Ameongeza kuwa, vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa na nafasi ya kimkakati katika jamii kutokana na kuweza kuitazama mihimili mingine ya dola  na kama inakwenda kinyume huweza kupaza sauti na vyombo vya habari haviwezi kupuuzwa hata kidogo kutokana na umuhimu wake katika utawala bora, uwazi na uwajibikaji.

Amesema,  taarifa ambazo huandikwa na vyombo vya habari zimekuwa zikisaidia katika masuala yenye usimamizi wa rasilimali za umma na katika Ofisi ya CAG na taasisi zingine. 

CAG amebainisha kuwa,katika ofisi hiyo kuna utaratibu  kila siku ambao umewekwa wa kufuatilia kila kilichoandikwa kwenye vyombo vya habari ili kubaini habari zilizoandikwa kuhusiana na rasilimali za umma na kwamba wanapoona habari imeandikwa hatua huchukuliwa kwa lengo la kusaidia kupata maeneo hatarishi kwenye usimamizi wa rasilimali za umma na kuandaa mpango kazi wa  ukaguzi katika maeneo hayo.

Amesema, wanapoona habari zimeandikwa katika vyombo vya habari  wamekuwa wakichumua hatua kwani taarifa hizo ni muhimu  sana katika kuhakikisha rasilimali za umma zinalindwa kwa manufaa endelevu huku akiwaomba wanahabari kuendelea kuandika habari hizo, kwani  ni wadau muhimu sana katika kusaidia rasilimali za umma ziwe na tija kwa taifa.

PICHA MBALIMBALI ZA WAHARIRI WA HABARI WAKIWA KWENYE MKUTANO HUO.



 

BAADHI YA WAHARIRI WA HABARI WAKIULIZA MASWALI.

Mhariri wa Gazeti la Mwananchi Lilian Timbuka akiuliza swali kwenye mkutano huo Jijini Dar es Salaam.

Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira Immanuel Mbuguni akizungumza alipokuwa akumuuliza maswali CAG (hayumo pichani) katika mkutano huo.

Maafisa kutoka Ofisi ya CAG wakifuatilia mkutano huo.



LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here