Home LOCAL HEDHI SALAMA BADO CHANGAMOTO KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MOROGORO.

HEDHI SALAMA BADO CHANGAMOTO KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MOROGORO.

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dokta Rita Liamuya akitoa elimu ya afya ya uzazi hasa alijikita katika hedhi salama kwa wananfunzi kutoka shule mbalimbali walioshiriki kwenye maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yalioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Chalice kwa kushirikiana na Save The Future Foundation (STFF) yaliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari ya Nelsonimandera.

Mratibu wa programu ya kutoka CHALICE Halifa Khan akizungumza katika maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yalioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Chalice kwa kushirikiana na Save The Future Foundation (STFF) yaliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari ya Nelsonimandera.
Wazazi na wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo.

NA: FARIDA MANGUBE.

Shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Morogoro zinakabiliwa na ukosefu wa miundombinu wezeshi kwa wanafunzi wa kike wenye umri wa kuingia hedhi ikiwemo ukosefu wa vyumba maalumu ya kubadilishia taulo, maji safi pamoja na tanuru za kuchomea taulo zilizotumika hali inayosababisha baadhi ya wanafunzi hao kushindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa hedhi.

Hayo yameelezwa kwenye maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yalioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Chalice kwa kushirikiana na Save The Future Foundation (STFF) yaliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari ya Nelsonimandera ambapo wanafunzi wa shule hiyo wamesema wanapata wakati mgumu wanaingilia kwenye hedhi jambo linaloasili maudhulio yao ya shule na kushindwa kufanya vizuri katika masomo.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dokta Rita Liamuya ameeleza madhara yanayosababishwa na hedhi isiyo salama ikiwa ni pamoja na kupata maradhi katika via vya uzazi vya mwanamke na kusababisha ugumba.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mratibu wa programu ya CHALICE halifa khan alisema wapo tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  wanapata hedhi salama ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Tupo katika mchakato wa kutengeneza taulo za kike za kufua ambazo zitagawiwa kwa shule za sekondari na msingi pamoja na kuwapa elimu mabinti juu ya hedhi salama.”alisema bwana Khan

Nae Mwenyekiti kituo cha tarifa na maarifa (TGNP) kutoka Kata ya Mkabarani Theresia Beregi ameiomba serikali kuweka bejeti ya taulo za kike katika shule za msingi kwani mabinti wengi wamekuwa wakianza kupata hedhi wakiwa na umri mdogo.

“Hapo awali mabinti walikuwa wanapata hedhi wakiwa na miaka kumi na mbili mpaka kumi na sita lakini siku hizi ni tofauti mtoto wa miaka tisa mpaka kumi anapata hedhi kimsingi huyo bado yupo shule  ya msingi.”alisema Bi Theresia

MWISHO.

Previous articleCAG AWATAKA WAHARIRI KUJIIMARISHA KATIKA HABARI ZA UCHUNGUZI
Next articleCHONGOLO AAGIZA KULETWA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA YA USHETU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here