Home LOCAL WANAWAKE NCHINI HAWAJANUFAIKA NA RASILIMALI ZINAZOPATIKANA KWENYE MISITU

WANAWAKE NCHINI HAWAJANUFAIKA NA RASILIMALI ZINAZOPATIKANA KWENYE MISITU


Mkuu wa Kituo cha Masomo ya Jinsia cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,Prof. John Jeckoniah akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari nje ya mkutano huo mara baada ya kuwasilisha matokeo ya utafiti wake.

Meneja Mradi , Charles Leonard akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu malengo ya Warsha hiyo.

Wadau na washiriki warsha hiyo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.



Warsha ikiendelea.

Wadau na Washiriki wa Warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.

Warsha ikiendelea.
Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea. 
 
Na: Calvin Gwabara, Morogoro

UTAFITI umeonesha kuwa Wanawake hawajanufaika sana ikilinganishwa na Wauame katika kufikia na kutumia rasialimali zinazopatikana kwenye  misitu ya asili kama vile uchomaji na biashara ya  mkaa,mbao pamoja na rasiliamali zingine zinazopatikana kwenye misitu hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kituo cha Masomo ya Jinsia cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof.John Jeckoniah mara baada ya kuwasilisha
matokeo ya utafiti wake uliokuwa unaangalia maswala ya Jinsia na makundi
maalumu katika utumiaji,ufikiaji na wanavyonufaika  na rasiliamali za misitu.

“Katika utafiti wetu tumebaini kuwa kuna changamoto kadhaa za kukosekana kwa uwiano wa kijinsia kwenye makundi maalumu yanyoshiriki katika kutumia rasiliamali za misitu ya asili ambapo imeonekana Wanawake hawanufaiki sana kama ilivyo Wanaume katika kufikia na kunufaika nazo” Alibainisha Prof. Jeckoniah.

Amesema kuwa katika utafiti wao walitakiwa kuangalia mikakati gani inayotumiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Mtamdao wa kuhifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG katika kubuni mikakati  mbalimbali za kuongeza ushriki wa makundi maalumu hasa
wanawake.

Prof. Jeckoniah amebainisha kuwa katika wamebaini kazi kubwa imefanywa na mashirika hayo katika kuwajengea uwezo na kuboresha Maisha na uchumi wa jamii kwenye vijiji mbalimbali vilivyofikiwa na miradi ya TFCG na Mjumita lakini mara nyingi maswala ya kijinsia huangalia zaidi Wanwake na kusahau Wanaume wakati nao wana mchango katika maamuzi na maoni kwenye familia.

Kufuatia utafiti huo wanaona Wanaume wakisahaulika kwenye mafunzo ya aina hiyo wakati wao ndio wanaotumika kutoa mawazo na maoni pamoja na usimamizi wa wake yako chini ya Wanaume hivyo wakisaulika wanweza kuwa kikwazo kwenye utekelezaji wake na kwenye maeneo mbalimbali Wanawake wamelalamika kuwa wanaume ndio kikwazo katika mabadiliko yao.

Akieleza malengo ya Warsha hiyo Meneja Mradi wa CoFOREST ambao unatekelezwa na shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) bwana Charles Leonard amesema lengo ni kuwashirikisha wadau na jamii matokeo ya tafiti mbalimbali saba zinazohusu uhifadhi wa misitu zilizofanywa na watafiti kupitia mradi wa CoFOREST.

“Lengo kuu ni kwanza wadau wapate uelewa wa matokeo ya tafiti hizo, lakini lengo la pili ni wadau wapate nafasi ya kuchangia na kutoa mapendekezo yao pamoja na kuchukua matokeo ya tafiti na kwenda kuyaingiza kwenye utekelezaji wa shughuli wanazozifanya katika kuhifadhi na kusimamia misitu hususani ya asili iliyo katika ardhi za vijiji nchini” Alibainisha bwana Leonard.

Ametoa Rai kwa Serikali pamoja na wadau walio kwenye sekta ya misitu hususani misitu ya asili  kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa misitu hiyo kuna haja ya kuangalia ni namna gani misitu hiyo inasimamiwa vizuri na kuzitumia rasilimali za misitu ya asili kwa kaisi abacho kitapalelea uharibifu wa misitu unaotokea kwenye misitu iliyo kwenye ardhi za vijiji ambayo haijahifadhiwa unakomeshwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here