Home Uncategorized POLISI WAISHIKA PABAYA SIMBA

POLISI WAISHIKA PABAYA SIMBA



Na: Stella Kessy.

MABINGWA watetezi Simba leo wameshindwa kupata matokeo dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliopigwa katika dimba la Ushirika Moshi.

Katika mchezo huo ambapo milango ya timu zote mbili ilikuwa migumu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo na kufanya timu zote zigawane pointi mojamoja.

Ubao umesoma Polisi Tanzania 0-0 Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa 19 msimu wa 2021/22.

Simba mpaka sasa wamefikisha alama jumla ya alama 41 wakiwa wameachwa kwa jumla ya pointi 10.

Yanga ni namba moja wana pointi 51 na wote wamecheza mechi 19 ndani ya msimu huu ambao kazikazi inaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here