Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brogedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 kwa Waandishi wa Habari(hawapo picha), unaotarajia kuanza mbio zake kesho mkoani humo ambapo utatembelea miradi 62 yenye thamani ya Shilingi bilioni 5,202,463,637.66 kati ya hiyo miradi 29 yenye thamani ya Shilingi bilioni 2,609,061,329.04 itafunguliwa,miradi 5 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1,511,397,430.00 itawekewa mawe ya msingi na miradi mingine 28 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1,082,004,878.00 itatembelewa na kukaguliwa.
JUMLA ya miradi 62 yenye thamani ya Sh. bilioni 5.202,463,637.66 inatarajiwa kutembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 katika mkoa wa Ruvuma.
Kati ya hiyo, miradi 29 yenye thamani ya Sh. bilioni 2,609,061,329.04 itafunguliwa,miradi 5 yenye thamani ya Sh.bilioni 1,511, 397,430.00 itawekewa jiwe la msingi na miradi 28 yanye thamani ya Sh. bilioni 1,082,004,878.00 itatembelewa/kukaguliwa pamoja na kugawa vifaa mbalimbali.
Mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema hayo leo ofisini kwake mjini Songea, wakati akitoa taarifa ya ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Waandishi wa Habari unaotarajia kuanza mbio zake mkoani humo kesho.
Alisema, Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika kijiji cha Lituhi Wilayani Nyasa ukitokea mkoa jirani wa Njombe kabla ya kuanza kukimbizwa katika Halmashauri ya wilaya Nyasa.
Aidha alisema,ukiwa mkoani Ruvuma Mwenge utakimbizwa umbali wa km 1,052.3 katika Halmashauri zote nane ndani ya wilaya tano za mkoa huo kuanzia tarehe 8 hadi 15 April.
Brigedia Jenerali Ibuge,amewaomba wananchi wa mkoa huo ambako Mwenge wa Uhuru utakimbizwa,kupita na kutoa ujumbe kujitokeza kwa wingi kusikiliza na kutoa ushirikiano kwa wakimbiza Mwenge na viongozi wengine watakaokuwa kwenye mbio hizo.
Pia Brigedia Jenerali Ibuge,amewataka wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanashiriki vyema zoezi la Sensa ya Watu na makazi linalotarajia kufanyika Mwezi Agosti Mwaka huu kwa kuhesabiwa na kutoa taarifa sahihi kwa makalani siku ya Sensa.
Amewakumbusha, wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Covid-19 kwa kuvaa barakoa,kunawa mikono na kunawa maji tiririka yenye sabuni.