Home LOCAL MAKAMU WA RAIS UCHAGUZI WA CCM KIGOMA

MAKAMU WA RAIS UCHAGUZI WA CCM KIGOMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipiga kura katika uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mbonimapaye Mpango akipiga kura katika uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Buhigwe mara baada ya kumaliza zoezi la uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wa CCM  wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

   

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza sera za wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma kabla ya zoezi la upigaji kura katika uchaguzi huo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango  amewaasa wananchi wa Kijiji cha Kasumo na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutumia fursa za miradi inayopelekwa na serikali katika mkoa huo  kikamilifu ili kujiletea maendeleo.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kigoma katika Kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mara baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura  katika uchaguzi wa  mwenyekiti na wajumbe wa CCM  wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga. Amesema serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika mkoa huo ikiwemo madaraja, barabara na ile ya elimu na kuwaasa wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata elimu inayotolewa bila malipo na serikali.

Aidha amewapongeza wananchi wa Buhigwe kwa kukubali kutoa eneo la hekari 149.9 kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha Tehama kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha songambele mkoani Kigoma.  Makamu wa Rais amesema serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa huo katika masuala ya miundombinu pamoja na mawasiliano.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewaasa viongozi wa shina namba 5 wa kitongoji cha kihanga kuongoza kwa weledi ili kuimarisha chama katika ngazi hiyo. Amesema viongozi  hao wa CCM wanapaswa kufanya vikao mara kwa mara ili kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya wananchi katika maeneo yao. Amesema ni muhimu viongozi wa CCM kuwa mstari wa mbele katika  kuimarisha umoja, upendo na ushirikiano katika jamii ikiwemo kuhamasisha uanglizi wa kila mmoja utakaoondoa uhalifu na matendo ya ukatili. Pia Makamu wa Rais amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha wanalipa ada za uanachama zitakazorahisha uendeshaji wa chama hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here