Home LOCAL MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI FUTARI NA KAMATI YA AMANI

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI FUTARI NA KAMATI YA AMANI

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kushiriki Futari iliondaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi wa Dini mbalimbali, Viongozi wa Serikali, Waumini pamoja na wananchi mbalimbali mara baada ya kushiriki Futari iliondaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 13 Aprili 2022 katika Viwanja vya Karimjee.

Sehemu ya Viongozi
  

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa dhehebu la Budha mara baada ya kushiriki Futari iliondaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 13 Aprili 2022 katika Viwanja vya Karimjee.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Viongozi wa Kisiasa pamoja na Mabalozi  mara baada ya kushiriki Futari iliondaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 13 Aprili 2022 katika Viwanja vya Karimjee.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewaomba viongozi wa dini nchini kujiepusha na migogoro ya ndani ya dini zao iinayosababishwa na kugombea uongozi pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati aliposhiriki Futari ilioandaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 13 Aprili 2022 katika Viwanja vya Karimjee. Amesema viongozi wa dini wanapaswa kutafuta kwa bidii na kuomba Amani itawale katika nyumba za ibada kwani migogoro ni kinyume na katiba za dini hizo pamoja na maandiko matakatifu.

Aidha Makamu wa Rais amewaagiza wakuu wa Mikoa kote nchini kuhakikisha wanaimarisha kamati za Amani ikiwa ni pamoja na kukutana na kamati hizo mara kwa mara. Makamu wa Rais amesema kamati hizo zimekua msaada mkubwa kwa kujenga maelewano baina ya viongozi na waumini wa dini mbalimbali, kuimarisha mawasiliano baina ya viongiozi wa dini pamoja na kuhimiza Amani kwa watanzania wote.

Pia Makamu wa Rais amewaomba viongozi hao wadini kutumia wakati huu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani pamoja na Kwaresma kuendelea kuliombea taifa na viongozi wake ili kuongoza kwa Amani na utulivu na kuyafikia maendeleo kwa haraka. Aidha amewaasa kuendelea kufundisha maadili mema katika jamii ili kuondoa matendo maovu na yakikatili yaliojitokeza siku za karibuni.

Kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ali amesema viongozi wa dini wataendelea kulipa kipaumbele suala la Amani hapa nchini na kuwakumbusha waumini kutambua kwamba suala la amani linapaswa kulindwa na sio kuchezewa.

Awali akisoma risala kwa Makamu wa Rais, Katibu wa Kamati ya Amani wa Mkoa wa Dar es Salaam Askofu Jackson Sosthenes amesema kamati imeeendelea kushirikiana kwa karibu na serikali katika kusimamia maadili ikiwemo  kupiga vita matendo maovu kama vile Rushwa, madawa ya kulevya pamoja na  biashara haramu za binadamu. Aidha ameongeza kwamba kamati tayari imejipanga kwa mwaka 2022 kushirikiana na serikali katika kuelemisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la  sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here