Home Uncategorized LIVERPOOL YAIFUMUA MAN UTD 4-0 DIMBA LA UNFIELD

LIVERPOOL YAIFUMUA MAN UTD 4-0 DIMBA LA UNFIELD

Timu ya Liverpool imeibuka na ushindi mnono wa jumla ya magoli 4-0 dhidi ya Manchester United ikiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliochezwa katika Dimba la Anfield nchini humo.

Mabao ya wababe hao wa Anfield yamepachikwa kambani na Luis Diaz katika dakika ya 5 ya mchezo huo huku Sadio Mane akitupia bao la pili katika dakika ya 68 ya mchezo huo. 

Mshambuliaji machachari kutoka Misri Mohamed Salah aliihakikishia ushindi wa mtanange huo timu yake kwa kupachika mabao mawili katika dakika ya 22 na 85.

Matokeo hayo yanaipa alama 76  Liverpool na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya England (EPL) na Manchester united yenyewe ikishuka mpaka.nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here