Home LOCAL HOFU YA KULIWA NA MAMBA WAKAZI WA KIJIJI CHA MKOKO YAONDOKA BAADA...

HOFU YA KULIWA NA MAMBA WAKAZI WA KIJIJI CHA MKOKO YAONDOKA BAADA YA KUPELEKEWA MRADI WA MAJI

Mkazi wa Kijiji cha Mkoko Jumanne Mavula akielezea jinsi alivyojeruhiwa na mamba baada ya kwenda kuchota maji Mto Wami mwaka 1991.

Moja ya wakazi wa Kijiji cha Mkoko akitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita wka uamuzi wake wa kupeleka mradi wa Maji Kijiji cha Mkoko mkoani Pwani.

Mmoja ya mafundi akiendelea na shughuli za ujenzi katika tanki la Maji Kijiji cha Mkoko.

Mkazi wa Kijiji cha Mkoko Jumanne Mavula(katikati) ambaye alipoteza sehemu ya mkono wake baada ya kujeruhiwa na mamba alipokwenda kuchota maji Mto Wami mwaka 1991 akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji uliopo kwenye kijiji chao ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka kwa mradi huo wa maji unaotekelezwa kwa fedha za UVIKO-19.

Mhandisi James Kionaumela akielezea kuhusu ujenzi wa tanki la maji unaendelea Kijiji cha Mkoko.

Mhandisi Yusuf Juma kutoka RUWASA Wilaya ya Bagamoyo (katikati)akifafanua jambo kwa viongozi wa Kijiji cha Mkoko(wanaosikiliza) kuhusu utekelezaji wa maji unavyoendelea katika kijiji hicho.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Mhandisi James Kionaumela akiangalia tofali zinazotumika katika ujenzi wa tanki linalojengwa katika mradi wa maji kijiji cha Mkoko.

Mhandisi James Kionaumela ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani (kushoto) akiwa na Mhandisi Yusuf Juma wakiangalia ujenzi wa tanki ambalo linaendelea kujengwa katika mradi wa Maji Kijiji cha Mkoko.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Mhandisi James Kionaumela (kushoto) akiangalia maelezo kwenye daftari akiwa na moja ya wahandisi walioko ndani ya wilaya hiyo baada ya kutembelea mradi wa maji Mkoko.

Moja ya vituo vya kuchotea maji kilichojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) Wilaya ya Bagamoyo kikiwa kimejengwa na kikamilika katika Kijiji cha Mkoko kilichopo Kata ya Msata wilayani humo.

Na: Mwandishi Maalum, BAGAMOYO.

TUNAMSHUKURU Rais Samia!Ndivyo wanavyoeleza wananchi wa Kijiji cha Mkoko kilichhopo Kata ya Msata wilayani Bagamoyo baada ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapelekea mradi wa maji.

Kwa mujibu wa wananchi hao wamesema kupatikana kwa mradi huo wa maji unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Bagamoyo kupitia fedha za UVIKO-19 unakwenda kuwaondolea hofu waliyonayo kwani watu wengi wamepoteza maisha na wengine kubakia na ulemavu wa kudumu kwa kujeruhiwa na mamba walipoenda kuchota maji mto Wami.

Wakizungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maji inayotokelezwa kwa fedha za UVIKO-19 , wananchi hao wamesema kupitia mradi huo wanakwenda kuondokana na adha ya kufuata maji mto Wami ambako wengi wao wamebakia na machungu ya kupoteza ndugu na jamaa zao wlioliwa na mamba walipokwenda kuchota maji na kuoga kwenye mto huo.

Mmoja ya wakazi wa Kijiji cha Mkoko ambaye alijeruhiwa na mamba mwaka 1991 alipoenda kuchota maji Mto Wami Jumanne Mavula amesema amefarijika kuona mradi wa maji kijijini kwao kwani ana uhakika watakuwa salama na hawatapata matatizo tena yakiwemo ya kujeruhiwa na kuliwa na mamba kama ilivyotokea kwake.

“Nilipoteza sehemu ya mkono wangu baada ya kujeruhiwa na mamba nilipoenda kuchota maji Mto Wami, mamba alinivuta mtoni akaanza kunishambuliwa, nilijitajidi lakini alifanikiwa kukata mkono wangu, hivyo nimebaki na kipande tu cha mkono tu.Hivyo ujio wa mradi huu wa maji katika Kijiji cha Mkoko  tunasema ahsante Rais Samia kwa kutumbuka na kuondolea adha ya maji iliyodumu muda mrefu.”

Akizungumzia mradi huo, Mwenyekiti wa kijiji cha Mkoko Mtoro Masimba ameelezea furaha waliyonayo baada ya kupatiwa mradi huo ambao muda si mrefu wananchi wataanza kupata maji ya bomba ambayo ni safi na salama.”Kijiji chetu kina wakazi zaidi ya 1,500 hivyo sote tutanufaika na mradi huu.”

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mkoko B, Jumanne Mdihile ameongeza kuwa Chama chao moja ya ahadi yao kwa wananchi kupitia Ilani ya Uchaguzi Mkuu wameahidi kuhakikisha watu wanapata maji karibu na makazi yao, hivyo utekelezaji wa mradi huo unaofanywa na RUWASA baada ya Rais Samia kutoa fedha inakwenda kutimiza ahadi kwa vitendo.

Amesema kwa muda mrefu wakazi wa Kijiji cha Mkoko wamekuwa wakitesaka katika suala la maji, na kwamba wengi wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa na mamba kwasababu ya kufuata maji Mto Wami, hivyo uwepo wa mradi huo unakwenda kufanya hata Chama kuendelea kuaminika kutokana na kutimiza ahadi zake.

Kwa upande wake Mhandisi James Kionaumela ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani amefafanua mradi huo unatekelezwa kwa fedha Sh.milioni 348 na zitatumika kusambaza mabomba ya maji yenye urefu wa  kilomita 16.2, ujenzi wa vituo tisa vya kuchotea maji na tenki la lita 50,000.

Ameongeza wananchi 1,742, watanufaika na mradi huo kwa kupata maji safi na salama .Ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 80 na tayari wamefikisha huduma za maji kwenye taasisi za elimu, dini na nyinginezo.

Kuhusu upatikanaji wa maji amesema kwa  Chalinze Vijijini maji yanapatikana kwa asilimia 69 na mijini asilimia ni 79 wakati matarajio ifikapo mwaka  2025 maji yawe yanapatikana kwa asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini na Mjini asilimia 95 na kwa jinsi wanavyotekeleza miradi watafikia asilimia hizo.

Mwisho.

IMEANDALIWA NA:Said Mwishehe Msagala, Michuzi TV.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here