Home LOCAL WAGANGA WA TIBA ASILI IGUNGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

WAGANGA WA TIBA ASILI IGUNGA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

 
Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora Sauda Mtondoo aliyeshika kamba yenye ng’ombe aliokabidhiwa kama zawadi na waganga wa tiba asili mkoa wa Tabora kwa ajili ya sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika kimkoa wilayani Igunga ikiwa ni moja ya kuunga mkono juhudi za serikali .

Na: Lucas Raphae,Tabora

Waganga wa Tiba asili wilayani Igunga mkoani Tabora , wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na uaminifu ili waendelee kuaminika katika jamii.

Hayo yalielezwa na mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo wakati akizungumza na waganga wa tiba asili Wilaya ya Igunga mjini Igunga.

Alisema waganga wa Tiba asili ni watu muhimu na wanapaswa kuaminika lakini lazima watekeleze Majukumu yao kikamilifu na kwa weledi mkubwa.

Mkuu huyo wa Wilaya pia amewataka watumie Umoja wao kufichuana kwa wale wanaokwenda kinyume na leseni zao na sio kusubiri wafichuliwe na Serikali

Aliwaeleza kuwa wanapaswa kujiepusha na naupigaji ramli chonganishi na kwamba wao wana umuhimu mkubwa katika jamii na pale inapotokea miongoni mwao akaenda kinyume wanakuwa wamepata sifa mbaya wote.

Kuhusu zoezi la Sensa la watu na makazi pamoja na chanjo ya Polio kwa watoto chini ya miaka mitano, amewataka kushiriki kikamilifu katika uhamasishaji ili wengi zaidi wajitokeze kuhesabiwa na watoto kupatiwa chanjo.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa waganga wa Tiba asilia, Uwata, mkoa wa Tabora, Ally Isike, Alisema watadhibitiana wao kwa wao na hawatasita kuwafichua wenzao wanaokwenda kinyume kwani wamesajiliwa kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na MIIKO ya kazi Yao.

Alisema wanataka kushirikiana na Serikali katika shughuli zake ikiwemo kusaidia kampeni ya kuhamasisha Sensa ya watu na makazi na kutoa elimu kwa jamii kutowaficha watoto wenye ulemavu ili nao wahesabiwe kwa kuwa ni haki yao ya msingi.

Aliahidi waganga kushiriki kampeni za kitaifa kwa vile wao wanakutana na watu wengi wakiwemo wateja wao wanaokwenda kupata huduma.

Isike aliomba nao kama Umoja wawe wanatoa mganga wa Tiba asili Bora kama watumishi wengine wa Serikali, Umma na watu binafsi.

Ombi hilo mkuu wa Wilaya Alisema analichukua na kulifanyiwa kazi na kuwa watapewa majibu kabla ya Mei Mosi.

Waganga hao wamechangia ng’ombe mmoja kwa ajili ya kamati ya maandalizi ya sikukuu ya wafanyakazi, itakayofanyika kimkoa Mei Mosi mjini Igunga.

Nao baadhi ya waganga waliohudhuria kikao hicho Maririka Masesa, Mwanzalima Mwisi na Mekrida Sayi walimshukuru mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo kwa ushirikiano ambao amekuwa akiutoa kwa waganga wa tiba asili na kusema kuwa nao wapo tayari kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yote ya serikali ikiwemo kuchangia miradi mbalimbali pindi watakapohitajika.

Umoja wa waganga wa Tiba asili umejipanga kushiriki shughuli za Serikali za kuhamasisha maendeleo kwa vile nao ni sehemu ya Jamii huku pia wakiahidi kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mwisho.

Previous articleHOFU YA KULIWA NA MAMBA WAKAZI WA KIJIJI CHA MKOKO YAONDOKA BAADA YA KUPELEKEWA MRADI WA MAJI
Next articleWWF YAZINDUA MPANGO WA ELIMU YA UHIFADHI NA MAZINGIRA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here