Home LOCAL CHONGOLO -CCM ITAENDELEA KUWEKA MSUKUMO KUHAKIKISHA MIUNDOMBINU INABORESHWA

CHONGOLO -CCM ITAENDELEA KUWEKA MSUKUMO KUHAKIKISHA MIUNDOMBINU INABORESHWA

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwahutubia Viongozi wa CCM Wilaya ya Kigamboni wakati wa Mkutano Maalum wa Halmashauri Kuu ya Wilaya kwenye ukumbi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwasili Kigamboni na kupokelewa na Viongozi wa CCM Wilaya ya Kigamboni ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukutana na Viongozi wa Chama katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amesema CCM itaendelea kuweka msukumo kuhakikisha miundombinu ya barabara na vivuko inaboreshwa Kwenye Wilaya ya Kigamboni kwa sababu ni lango la uchumi wa Taifa.

Amesema kwa sasa asilimia 90 ya bidhaa ya mafuta yanayotumika nchini yanategemewa kutoka Kigamboni na magari kutoka mikoa tofauti yanaenda kuchukua bidhaa hiyo na kusambaza lakini kumekuwa na changamoto ya foleni namna ya kulifikia eneo hilo.

Akizungumza akiwa Wilayani hapo kwenye muendelezo wa ziara ya kufuatilia mchakato wa uchaguzi ngazi ya mashina, alisema kutokana na changamoto hiyo Chama hicho kinachukua hatua ya kwenda kujadiliana na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kuangalia namna ya kuboresha miundombinu hiyo.

“Tunaona Kasi ya ukuaji wa Kigamboni na magari yamekuwa mengi na yanachukua hadi muda wa masaa matatu kulifikia na kutoka Kurasini, naondoka na changamoto hii naenda kuongea na (Tanroads) na (Tarura)kuona namna ya kuboresha barabara, kwakuwa Kigamboni nilango la uchumi,” alisema

Katika maelezo yake amesema CCM bado inajipanga ilikuja na Suluhu ya kudumu kuboresha vivuko huku akieleza hata changamoto ya daraja la Julius Nyerere walishaipokea na wanaendelea kuishughulikia.

“Changamoto zote tunazibeba na tunaiangalia
Kigamboni kwa jicho la tatu,tutajenga barabara kuanzia kibada itakatisha Kisarawe II ,Pemba mnazi hadi Mbagala,”amesema

Chongolo amesema kuhusu changamoto ya vivuko ametoa maagizo Kwa Mamlaka husika kutengeneza vivuko vikivyoharibika kwani vivuko hivyo si anasa bali ni huduma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here