Home LOCAL WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA QATAR, JORDAN

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA QATAR, JORDAN

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini kwenda Qatar na Jordan kwa ziara ya kikazi.

Akiwa huko, Waziri Mkuu atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika vikao na viongozi wakuu wa nchi hizo.

Tanzania na Qatar zimepanga kuanzisha Tume ya Ushirikiano ya Pamoja ambayo itasimamia masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo na usafiri wa anga.

Akiwa Jordan, Waziri Mkuu atashiriki mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan Msumbiji na maeneo jirani. Mkutano huo wa Aqaba Process on East Africa, utafanyika Machi 24, 2022 katika mji wa Aqaba, Jordan.

Mkutano huo ambao umeitishwa na Mfalme wa Jordan, Mheshimiwa Abdulla wa II ni wa tatu kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 na huwakutanisha viongozi wakuu wa nchi za ukanda wa Mashariki ya Afrika ili kujadili changamoto za ugaidi na namna ya kudhibiti.

Previous articleNAIBU WAZIRI UMMY NDELIANANGA AKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO JIJINI DODOMA
Next articleSERIKALI YAVUNA BI;.540 KUTOKA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here