Home BUSINESS WAKALA WA MBEGU NCHINI ASA WATAKIWAA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBEGU...

WAKALA WA MBEGU NCHINI ASA WATAKIWAA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBEGU BORA



Na: Lucas Raphael Dodoma

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof Siza Tumbo amewataka Wakala wa Mbegu nchini ASA ,kuhakikisha wanatoa elimu ya matumizi bora ya mbegu kwa wanunuzi na wakulima ili kuongeza asilimia ya watumiaji wa mbegu borazinazosambazwa na wakala huyo nchini

Alitoa Kauli hiyo alipokuwa  akifungua kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wizara ya Kilimo Dodma baina ya Wakala wa mbegu nchini (ASA) na wasambazaji walioingia mkataba wa kusambaza mbegu na wakala huyo,

Alisema kwamba Wakala anapaswa kuongeza jitihada katika usambazaji ili kuongeza idadi ya wakulima wanaotumia mbegu bora.

Prof Tumbo alisema takribani asilimia 10 ya wakulima wanaotumia mbegu bora ambazo zimeboreshwa hivyo wasambazaji wa mbegu mnapaswa kuwa maafisa ugani kuwaelimisha wanunuzi umuhimu wa matumizi ya mbegu bora,jambo litalaochangia kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima kwa kutumia mbegu bora za mazao.

Ni asilimia chache ya wakulima wanaotumia mbegu bora za wakala wa uzalishaji mbegu,hivyo mnapaswa kuongeza bidii ya kusambaza mbegu kwa wakulima pamoja na kuwapa elimu ya kuzitumia,”alisema Naibu Katibu Mkuu.

Alifafanua zaidi ya kuwa idadi ya watumiaji wa mbegu bora ikiongezeka,basi hata soko litakuwa kubwa kwa wakulima kutokana na kwamba,wakulima hao watakuwa na uzalishaji wa kutosha katika mashamba wanayozalisha mbegu hizo.

Prof Tumbo akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mazao wenye tija ambao unaleta matokeo chanya,alisema mkulima anatakiwa kuwa na viauatilifu,mbolea,mbegu bora na vitu vingine ambavyo vitamsaidia mkulima kuboresha shamba lake kabla na baada ya msimu wa mavuno.

“mpaka leo hii bado wakulima wanahangaika na uzalishaji wa mahindi kutokana na kutofuata taratibu za kilimo bora kitendo kinachochangia kupata tani chache za mahindi kwa heka moja ya shamba,ukilinganisha na mkulima anayefuata matumizi bora ya kilimo “alisema Prof Tumbo.

Alisema,wakulima wakizingatia kufuata kanuni bora za kilimo,watasaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa uzalishaji wa mbegu bora ambazo zitaleta tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

Alisema serikali kila wakati  wanasisitiza suala la matumizi ya mbegu bora ,Viuatilifu zana za kilimo kwa sababu vitu hivyo ukiwa navyo na wakijua kuvitumia vizuri wanaweza kupata mazao yale ambayo tunasema wanazalisha kwa tija.

Naye Mtendaji mkuu wa ASA,Dkt Sophia Kashenge alisema maelekezo waliopewa na Wizara watayafanyia kazi kikamilifu ikiwemo kuhimiza wadau

wasambazaji wa mbegu katika maeneo ya pembezoni kuongeza bidii yankuwafikishia wakulima kwa wakati wote hasa msimu wa Kilimo

Alisema moja ya changamoto ambayo inawasumbua wakulima ni ucheleweshaji wa mbegu,hivyo hilo watalifanyia kazi ili kuhakikisha wanaboresha hilo,ambalo anaamini litasaidia kutatua changamoto .

Hata hivyo alisema kikao hicho na wadau wasambazaji wa mbegu ambao wameingia mkataba wa kusambaza mbegu kwa wakulima,kitasaidia kuimarisha Ushirikiano baina yao,kutokana na kwamba sasa hivi serikali imeelekeza nguvu katika kufanya kazi na sekta binafsi.

“Tunaishkuru serikali kwa kuamua kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi,hili litaongeza ufanisi katika usambazaji wa mbegu,”alisema Dkt

Kashenge.

Alisema wanapofanya kazi pamoja na sekta binafsi,wanaongeza wigo wa utendaji,ambapi  kiu yao ni kuhakikisha usambazji wa mbegu unaongezeka kwa kiasi kikubwa ili mkulima asipate tabu ya kupata mbegu,pindi msimu wa kilimo unapowadia.

 

Mwisho.


 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here