Na:Costantine James, Geita.
Mamlaka ya mapato nchini Tanzania TRA mkoa wa Geita imejipanga kukusanya mapato kiasi cha shilingi Bilioni 37.7 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo kuna ongezeko la bilioni 5.7 ukilinganisha na kiasi ambacho ilikuwa imepangiwa kukusanya kwa mwaka wa fedha uliopita 2020/2021.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa mamlaka ya mapato nchini Tanzania ( TRA) Mkoa wa Geita, Hashim Ngoda amesema TRA mkoa wa Geita imejipanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 37.7 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Ngoda amesema TRA mkoa wa geita imekuwa na mwenendo mzuri wa ukusanyaji wa mapato katika mkoa huo kwani maranyingi wamekuwa wakifikia kiwango ambacho wamepangiwa kukusanya kwa mwaka husika.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 walifanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 96% hali ambayo inawafanya wawe ni miongoni mwa mikoa nchini Tanzania inayofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato hapa nchini.
Aidha amesema mpaka kufikia mwezi juni lengo walilopangiwa la kukusanya Bilioni 37.7 watakuwa wameshafanikiwa hali inayowafanya kutimiza malengo ya kukusanya mapato kwa mkoa wa Geita kwa lengo la kuiwezesha serikali kuendesha miradi mbalimbali ya kimaendeleo kupitia kodi zinazo kusanywa na mamlaka hiyo.
“Mwaka huu wa fedha mhe. Mkuu wa mkoa tunalengo la kukusanya kiasi cha Bilioni 37.7ambalo ni sawa na ongezeko la bilioni 5.7 ukilinganisha na lengomla mwaka 20201/2021, kwa kipindi cha miezi 8 mkoa umefanikiwa kukusanya bilioni 21 sawa na asilimia 88.4, mkuu wa mkoa tukuhakikishie kwamba hadi kufikia huji lengo tulilo pangiwa la bilioni 37.7 tutakuwa tumelifikia” Amesema Hashim Ngoda Meneja wa TRA mkoa wa Geita.
Hata hivyo meneja wa TRA mkoa wa Geita amesema katika kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali wana kampeni inayoitwa “kama wote”, yenye lengo la kuwakamata mtu asiye toa risiti pamoja na anenunu bidhaa bila kudai risiti kwani kwa kufanya hivyo itahimiza na kuongeza kasi ya matumizi EFD mashine.
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe Rosemary Senyamule amewapongeza TRA mkoa wa Geita kwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ndani ya mkoa wa Geita kwani ukusanyaji wa mapato vyema unaiwezesha serikali ya Tanzania kuwa na uchumi mkubwa.
Hata hivyo Mhe, Senyamule ametumia nafasi hiyo kuwataka wanyabiashara pamoja na wakazi wa mkoa wa Geita kwa ujmla kujikita zaidi katika matumizi ya EFD mashine pale wafanyabiashara wanaopo uza bidhaa zao huku akiwataka pia wanunuzi kudai risti kwani ni haki yao na kufanya hivyo kutaiwezesha TRA kusanya mapato kiasi ambacho wamepangiwa huku akisema nchi inaendeshwa kwa mapato ya kodi.
Vile vile Mkuu wa mkoa amewataka TRA mkoa wa Geita kubuni ama kutumia njia nzuri za kukusanya mapato kwa weredi na maarifa ikiwemo kutoa elimu ya kutosha kwa wafanya biashara kwani kutoza kodi kwa shuruti sio mpango endelevu wa ukusanyaji wa mapato kwa wafanya baishara.
“kufanya watu walipe kodi kwa sababu wameelewa faida ya kodi na mioyo yao imesema lazima tuendeleze nchi yetu ni mtindo ambao ni endelevu na utaiwezesha nchi kustawi na kukua kwa sababu kila mutu atakuwa amejua faida” Amesema Rosemary Senyamule Mkuu wa mkoa wa Geita.