Home SPORTS WAZIRI MCHENERWA AMTUNUKU ZAWADI YA MFANO WA MELI MAHER ZAIN

WAZIRI MCHENERWA AMTUNUKU ZAWADI YA MFANO WA MELI MAHER ZAIN

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amemkabidhi zawadi ya mfano wa meli mwanamuziki maarufu  Duniani mwenye asili ya Lebanoni Maher Zain kutoka nchini Sweden anayejulikana kwa Nyimbo za Kaswida, kama sehemu ya kuhamasisha utalii hapa nchini.

Waziri Mchengerwa amemkabidhi zawadi hiyo  katika tamasha la siku moja lililofanyika usiku wa Machi 12 jijini Dar es Salaam, maalum kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa  vyombo vya usafiri na kukuza kipato kwa walemavu wasio ona  wanaolelewa katika kituo cha Vimdat kilichoko Kisemvule jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya mashabiki wake waliofurika kuburidika na nyimbo zake kabla ya kuhitimisha tamasha hilo, mwanamuziki huyo maarufu wa Qaswida duniani aliyevalia tisheti yenye maneno (Tanzania Unforgettable) amesema uwepo wake Tanzania ni jambo asiloweza kulisahau Maishani mwake kutokana na uzuri wa Tanzania na ukarimu wa watu wake.

“Naishukuru Serikali ya Tanzania na ninakupongeza Mheshimiwa Waziri kukuona hapa na wewe umekuja kuburudika na nyimbo zangu kweli Tanzania siyo ya kusahulika” alisme Maher

Akizungumza kwa niaba ya waandaji wa tamasha hilo Mwenyekiti msaidizi Yousra Alnahd amesema tamasha hilo lililopewa jina la Maher Zain in Tanzania pamoja na mapato ya tamasha hilo kulenga ununuzi wa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kituo hicho, pia waandaji walilenga kuitangaza utalii kama sehemu ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu katika kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.

Mwisho.

Previous articleTRA GEITA YAJIPANGA KUKUSANYA BILIONI 37.7.
Next articleWAHENGA ALUMINIUM WACHANGIA SH 500,000 WANAWAKE WA MINAZI MIREFU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here