Home SPORTS SIMBA SC YAIADHIBU BIASHARA 3-0 KWA MKAPA

SIMBA SC YAIADHIBU BIASHARA 3-0 KWA MKAPA

Na: Mwandishi wetu.

MABINGWA watetezi Simba leo wameendeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa  Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Biashara United usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba  leo yamefungwa na kiungo  wa timu hiyo Pape Sakho katika dakika ya 8 bao la pili limefungwa na Mzamiru Yassin katika dakika ya 13, na katika dakika ya 18 Clatus  Chama aliipatia timu yake bao la tatu.

Simba leo imeendeleza wimbi lake la kuondoka na ushindi mnono  na kufikisha alama 34 na jumla ya mechi 16 na kikosi kipo katika nafasi ya pili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here