Home BUSINESS SERIKALI YAWAITA WADAU KUTOA MAONI YAO RASIMU YA SERA MPYA YA UWEKEZAJI...

SERIKALI YAWAITA WADAU KUTOA MAONI YAO RASIMU YA SERA MPYA YA UWEKEZAJI JIJINI DAR

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ally Gugu akizungumza alipokuwa kwenye mahojiano maalum na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wadau wa kupata maoni ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 2022 Jijini dar es salaam.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti TPSF Andrew Mahiga akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari juu ya Sekta hiyo ilivyojipanga kikamilifu katika kuhakikisha wadau wanajitokeza kutoa maoni yao katika rasimu hiyo

Mshauri Mwelekezi wa rasimu hiyo Prof. Samwel Wangwe akitoa mada katika mkutano huo

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti TPSF Andrew Mahiga (wa pili kulia) akiwa na wadau wengine walipokuwa wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mshauri wa kuratibu rasimu hiyo Prof. Samwel Wangwe leo Jijini Dar es salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Katika kuhakikisha wawekezaji wanakuwa na mazingira bora na salama katika shughuli za Uwekezaji na Biashara hapa nchini, Serikali imewaita wadau mbalimbali katika Sekta ya uwekezaji ili kupitia rasimu ya mabadiliko ya Sera ya Uwekezaji kwa kupata maoni yao yatakayowezesha kufanya maboresho katika Sera iliyopo.

Akizungumza leo Ijumaa Machi 18,2022 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua  Mkutano wa wadau wa kupata maoni ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 2022,   Naiba Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  Ally Gugu amesema kuwa serikali imedhamilia kuendeleza juhudi za kuongeza imani kwa wawekezaji ili kuchangia ukuaji wa uchumi.

Amesema kuwa wadau hao wamekutana ili kutoa maoni yao ya mabadiliko ya sera, sheria na kanuni zinazosimamia uwekezaji kwa lengo la kuwavutia wawekezaji pamoja na kuondokana na urasimu katika utoaji wa vibali vya kufanya kazi na kuidhinisha miradi ya uwekesaji na kuisaidia serikali kutengeneza ajira zisizopungua milioni nane katika kipindi cha miaka mitano kunzia 2020 – 2025.

“Leo tumekutana na wadau wakiwemo Sekta Binafsi kwaajili ya kujadili na kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Uwekezaji tunafahamu kwamba Sera iliyopo sasa ni ya mwaka 1999 sasa yapo masuala mengi ambayo yanahitaji kupitiwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye Sera ile ikiwemo kuanzishwa kituo cha uwekezaji nchini ambacho kimeweza kuzaa miradi zaidi ya 10,000, lakini bado zipo changamoto kadhaa zinazohitajika kufanyiwa kazi” amesema Naibu Katibu mkuu Gugu.

Na kuongeza kuwa “kutokana na utekelezaji wa mipango mikakati mbalimbali ya kuboresha mazingira ya uwekezaji serikali imefanikiwa kuanzisha kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mwaka 1997 ambapo hadi Desemba 2021 kimefanikiwa kusajili miradi 10,838” Ameongeza.

Aidha ameeleza kuwa inakadiriwa miradi ya kiasi cha mtaji wa dola za marekani bilioni 103.05 itawekezwa, na kwamba kumekuwepo uratibu mzuri wa masuala ya uwekezaji kwa kuanzishwa idara maalum ya kuratibu maendeleo ya uwekezaji ndani ya wizara yenye dhamana ya Uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Utafiti TPSF Andrew Mahiga, amesema kuwa Sekta Binafsi imejipanga vema kuhakikisha wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wanatoa michango yao katika rasimu hiyo ambayo ni mhimili mkubwa wa Sekta hiyo katika kuimarisha wekezaji na Biashara hapa nchini.
 
“Sisi kama Sekta Binafsi tuna matarajio makubwa sana kuwa kutakuwepo na Sera itakayotambua Mchango wa Sekta Binafsi kama msingi wa uchumi pamoja na kuhamasisha Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi” Ameeleza Mahiga


Naye Mshauri Mwelekezi wa rasimu hiyo Prof. Samwel Wangwe, amesema kuwa Sera ya mwaka 2022 inakwenda kuweka mazingira mazuri ya Uwakezaji wa ndani na kwamba ana imani kubwa na wadau wote watakaofikiwa na rasimu hiyo watakwenda kutoa mawazo yao kwa kuangalia masilahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.

“Lengo ni kupata mawazo kutoka kwa wewekezaji ili kuhakikisha inakuwa na mazingira rafiki kwa kuzingatia ukuzaji wa kiuchumi na kuchangamsha sekta nyengine” amesema Prof. Wangwe.

Mwisho.

 
PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI WA MKUTANO HUO.

  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here