Home LOCAL RC GEITA AWATAKA BODABODA GEITA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOT

RC GEITA AWATAKA BODABODA GEITA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOT

Na:Costantine James, Geita. 

Mkuu wa Mkoa wa  Geita Rosemary Senyamule amewataka waendesha pikipiki Maarufu kama bodaboda kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Mkoa wa Geita.

Ameyasema hayo wakati  wa zoezi la kufungua  mafunzo ya ukatili wa kijinsia kwa waendesha pikipiki  maarufu kama Bodaboda 200 kutoka Geita  wanaoshiriki mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia  yanayoendeshwa na shirika la  Plan international  kwa wa siku tatu mkoani Geita.

Senyamule amesema shirika la Plan International limefanya  jambo zuri kwa kutoa elimu kwa bodaboda juu ya mambo ya ukatili wa kijinsia hasa unyanyasaji wa mtoto.

Waendesha bodaboda ni kundi mhimu sana katika kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwani  kundi hilo linafanya kazi ambayo inawakutanisha na kila aina ya watu wakiwemo na watoto.

Senyamule amelishukuru shirika la Plan International kwa kutoa elimu hiyo kwa bodaboda ametumia nafasi hiyo kulitaka shirika hilo kupanua wigo wa utoaji wa elimu kwa makundi mbali mbali ya kijamii kwa lengo la kutokomeza unyanyasaji wa kijisia hasa kwa watoto.

Awali  Meneja wa shirika la Plan International mkoa wa Geita  Adolf Kaindoa  wakati akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mmoa amesema  shirika hilo limeamua kutoa mafunzo kwa bodaboda kutokana na utafiti wao kuonyesha kuwa kuanzia Januari 2021 hadi Machi 2022 kulikuwa na kesi za ukatili wa kijinsia 22 zilizoripotiwa Ofisi ya ustawi wa jamii zikiwahusisha  waendesha bodaboda.

Adolf ameongeza  kuwa shirika la Plan international mpaka sasa limetoa kadi za  bima ya afya zilizo boleshwa kwa watoto 7400 ndani ya mkoa wa Geita.

Aidha Adolf amesema wao kama Plan international wataendelea kutoa mafunzo katika makundi mbalimbali kwa lengo la kutokomoeza ukatili wa kijinsia huku akisema mafunzo wanayotoa kwa bodaboda katika kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia yanafanyika kwa siku tatu.

Ulinzi na usalama ni jumu letu sote hivyo tuungane kwa pamoja kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto kwani watoto wa leo ndo taifa la kesho wewe na mimi sema ukatili kwa watoto sasa basi.

Previous articleOFISI YA RAIS-UTUMISHI YDHAMIRIA KUWA YA KWANZA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA KUDUMU KATIKA MJI WA SERIKALI ILI KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI
Next articleHABARI KUTOKA MAGAZETINI ASUBUHI YA LEO IJUMAA MACHI 25-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here