Home SPORTS POLISI TANZANIA YAPANIA KUFUFUKIA KWA AZAM.

POLISI TANZANIA YAPANIA KUFUFUKIA KWA AZAM.

Na: mwandishi wetu

KIKOSI cha Polisu  Tanzania kinatarajia kushuka tena katika dimba la Azam Jumamosi hii kuwakabili  Azam katika mchezo wa ligii kuu ya NBC utakaochezwa kuanzia saa 1 usiku.

Kuelekea mchezo huo Polisi Tanzania itashuka dimba ikiwa haina mwenendo wa kuridhisha kwa siku za karibuni kutokana na rekodi ya kupoteza michezo 3 na kupata sare 2 na kuwa na alama 19 ikishika nafasi ya 9 kwenye ligi inayoendelea sasa.

Akizungumza na blog hii ya Green waves media  kuelekea mchezo huo msemaji wa timu hiyo Hassan Juma amesema mchezo wao na Azam hautakuwa mwepesi kutokana na kuwa timu zote mbili kwenye michezo yao miwili ya hivi karibuni wamepoteza na kutoka sare. 

Juma ameongeza timu yao haijawahi kupata matokeo katika ligii kuunya NBC tangu walipoifunga Prison mwezi Desemba kwenye ushindi wa goli 1 uwanja wa ushiriki hivyo mchezo wa Jumamosi watakwenda kuikabili Azam kwa lengo moja tu la kuwapa furaha mashabiki wao ambao wamekosa kwa kipindi kirefu.

“Tunakwenda kuwakabili Azam tukijua ugumu wa mchezo unaotokana na timu yao kwanza kutaka kulipa kisasi cha mchezo uliopita lakini pia nao michezo miwili ya mwisho matokeo yao siyo ya kuridhisha sana hivyo hatutodharau mchezo huu kwa kuwa tukipoteza tutaruhusu Azam kutukimbia kwa idadi kubwa ya alama hivyo kupelekea ugumu kwenye safari yetu tuliyokusudia kumaliza nafasi 3 za juu”.

Polisi Tanzania itashuka kwenye uwanja huo ikiwa na kumbukumbu ya kudondosha alama tatu baada ya kupokea kipigo cha magoli 3 kwa 0 toka kwa KMC ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa timu ya KMC ikipata mbele ya Polisi Tanzania kwenye michezo 6. 

Katika mchezo wa duru la kwanza ulimalizika kwa  Polis Tanzania na Azam, Polisi kutoka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 kwenye dimba la Ushirika magoli ya Kassim Haruna na Adam Adam ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi cha Polisi kwenye mchezo huu wa marudiano kutoka na matatizo ya kifamilia  aliyonayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here