Home SPORTS NGWANDO, KIBAZANGE KUGOMBANIA UBINGWA PST KESHO CHAMPION KITAA

NGWANDO, KIBAZANGE KUGOMBANIA UBINGWA PST KESHO CHAMPION KITAA

Na: Stella Kessy, DAR

BONDIA wa ngumi za kulipwa Ally Ngwando na James Kibazange kesho wanashuka dimbani kuchuana katika kuwani mkanda wa ubingwa wa PST katika pambano la litakalopigwa kesho kwenye Fainali ya Championi wa Kitaa.

Akizungumza leo wakati mabondia 32 wakipima uzito kuelekea fainali ya Champion kitaa promota wa ngumi za kulipwa Meja Seleman Semunyu amesema kuwa ametoa ofa ya mkanda huo katika pambano hilo ambalo litapigwa kwa raundi nane.

Ameongeza kuwa katika pambano hilo limeonekana kuwa na   upinzani mkali kutokana na mitaa wanayotokea mabondia hao ambao walifika katika kupima uzito wakiwa na kundi kubwa la mashabiki wao huku kila upande ukitamba kumchapa mpinzani wake.





Hata hivyo Meja Semunyu amewaomba mashabiki waliojitokeza  kwenye uzito leo ikiwa kesho wataweza kuujaza Uwanja wa ndani wa Taifa ya basi atawatangazia zawadi nyengine.

Kwa Upande wa James Kibazange amesema kuwa amejiandaa vyema kwa pambano hilo ambalo yeye analichukulia kama pambano la ushindi.

“Nipo vizuri kuelekea pambano hilo na sintamwacha mpinzani wangu apumue kwani nitaibuka na ushindi wa Tko mapema sana ninaomba wadau na mashabiki wangu kujitokeza kwa wingi kesho katika pambano hilo ambalo nitakuwa la kipekee” amesem 

 

Huku upande wa bondia Ally Ngwando amesema hana maneno mengi ila amehaidi kuibuka na ushindi kwani amejiandaa vya kutosha kuelekea katika fainali.

“Sina maneno mengi kikubwa nataka wadau na mashabiki wangu kujitokeza kwa wingi kuja uwanjani  kwani ninampa tahadhari kubwa kwa maandalizi  niliyojiandaa ninauhakikika pambano hili amalizi  yeye na Kocha wao wajindae kwani wasije pata shida kesho” amesema.

 

 

Previous articleNAIBU WAZIRI MHE. MWANAIDI AZINDUA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU UKATILI WA WATOTO MTANDAONI, WADAU WAFUNGUKA.
Next articleGEITA WAMKOSHA NAIBU WAZIRI KWA KUTEKELEZA ZOEZI LA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here