Home LOCAL IGP SIRRO AWAGIZA MAKAMANDA KUFANYA OPERESHENI MWEZI MMOJA BARABARANI

IGP SIRRO AWAGIZA MAKAMANDA KUFANYA OPERESHENI MWEZI MMOJA BARABARANI

 DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaagiza Makamanda wa Polisi nchi nzima kufanya operesheni ya mwezi mmoja ya kudhibiti makosa ya usalama barabarani ambayo kwa kipindi cha mwezi wa tatu mwaka huu yameonekeana kuongezeka.

IGP amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kikao kazi na Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Rufiji ma RTOs na DTOs pamoja na Wakuu wa Operesheni kutoka kwenye mikoa hiyo.

Aidha, katika kikao kazi hicho IGP Sirro ametoa agizo kwa wananchi kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuepusha ajali zinazoweza kuepukia.

Katika hatua nyingine IGP Simon Sirro amekutana na kuzungumza na balozi wa Palestina nchini Tanzania Mhe. Hamdi Mansour Abuali aliyemtembelea ofisini kwake Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo na kujadiliana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama na ushirikiano.

Previous articleMWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM,RAIS WA TANZANIA MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU PAMOJA NA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA JIJINI DODOMA
Next articlePROF. MAKUBI AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA KUFUATA MIONGOZO YA UNUNUZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here